Wednesday, August 31, 2011

Rais wa Zanzibar Dk.Ali Shein Ahudhuria Swala ya Idd el Fitri Bwawani Hotel Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akiwahutubia wananchi na waislamu katika baraza la Iddi el Fitri lililofanyika huko ukumbi wa Salama hall Bwawani Hotel mjini Zanzibar.
Makamo wa kwanza wa Rais Seif Sharif Hamadi akisalimiana na Waziri wa katiba na Sheria wa Zanzibar Abubakari Khamis Bakari baada ya kuingia katika kiwanja cha maisara mjini zanzibar kwa ajili ya kuswali swala ya Idi Elfitri.
Rais wa Zanzibar Alhaji Dr,Ali Mohd Shein pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali na wananchi,wakiwa katika swala ya iddi ambayo imeswaliwa kitaifa katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.
Baadhi ya kinamama waliohudhuria katika swala ya Idi Elfitri huko katika kiwanja cha Maisara mjini Zanzibar
 Wananchi mbalimbali wa Zanzibar wakisikiliza hotuba ya Idi Elfitri baada ya kumaliza kuswali swala ya Idi huko katika kiwanja cha maisara zanzibar.Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu -Zanzibar

Rais Jakaya Kikwete Ashiriki Swala Ya Iddi Msikiti Wa Kichangani,Magomeni Mapipa DSM

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu waumini waliohudhuria swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Iddi katika msikiti wa kichangani uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam leo asubuhi
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa mkono wa Iddi baadhi ya waumini waliohudhuria swala ya Iddi katika msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Picha zote: Freddy Mar-IKULU

Monday, August 29, 2011

mbunge Wa Mvomero Aingilia Kati Mgogoro Wa Ardhi Kipera

M

|
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makala akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, Morogoro mwishoni mwa wiki katika harakati za kutatua mgogoro wa ardhi uliopo kijijini hapo , kufuatia mwekezaji Raia wa kigeni kuuziwa eneo kubwa la ardhi na kumega sehemu ya mashamba yao, kufunga barabara, shule na kubomoa baadhi ya vyoo vya wakazi wa kijiji hicho. MBUNGE wa jimbo la Mvomero, mkoani Morogoro, Amos Makala ameingilia kati mgogoro wa ardhi uliopo katika Kitongoji cha Kinyenze , Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali , Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro baina ya wananchi na mwekezaji wa Kigeni aliyeuziwa shamba kijijini hapo.

Akizungumza mwishoni mwa wiki Kijijini hapo Makala aliyeambatana na Ofisa Ardhi wa Wilaya hiyo, Majaliwa Jaffari amewataka idara ya ardhi kuchukua hatua za haraka na dharula kutatua mgogoro huo kabla ya kuibuka kwa machafuko ya uvunjifu wa amani.

“Nimejionea mwenyewe baada ya kusikia kiliochenu juu ya mwekezaji huyu, watu wa ardhi tafadhalini sana lishughulikieni suala hili haraka sana na mkae pamoja mgogoro huu umalizike upesi iwezekanavyo, ndani ya wiki moja tatizo hili liwe limemalizika”, alisema Makala.

Aidha Makala amesema tatizo hilo likiendelea ataungana na wananchi wake kufungua kesi Mahakamani ya kumpinga mwelezaji huyo na amemwomba Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero kutumia mamlaka waliyonayo kufika kijijini hapo wafungue uzio huo uliowekwa na mweklezaji huyo haraka ili kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali, watoto kwenda shule na watu kuvuna mazao yao yanayoibiwa na walinzi wa kampuni ya Tanbreed Poultry Limited ambayo imemega mashamba yao.

“Katika hili ninaungana nanyi na Viongozi wa Mkoa na Wilaya wafike hapa wakiwa na dola na kukata uzio huu, ili wananchi muendelee na shughuli zenu za kijamii, si haki kufunga barabara mnayoitumia kwenda katika makazi yenu na mashambani, hili lisipofanyika tutatafuta mwanansheria na kufungua kesi ya Mahakamani ya kumpinga mwekezaji huyu”,alisema Mbunge Makala.

Makala pia aliwapongeza wakazi wa kijiji hicho kwa kuwa watulivu pasipo kufanya vurugu katika kipindi kirefu tangu kuibuka kwa mgogoro huo bila kupatiwa ufumbuzi kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu licha ya kuandikiwa barua tangu mwezi Aprili mwaka huu mgogoro huo ulipoanza kushika kasi.

“Wananchi mmefanya jambo jema sana la kuheshimu mamlaka za kisheria kwa kuwa watulivu kipindi chote lakini vinginevyo hapa machafuko yangetokea maana wananchi mpo wengi kuliko hao askari wao wanaolinda hilo shamba”, alisema Makala.

Pia alisema kwa maelezo aliyoyasikia kutoka kwa baadhi ya wazee wa kijiji hicho Ally Kidunda na Said Ahmad na viongozi wa Kijiji yaliyotolewa kwaa nyakati tofauti Mwekezaji huyo ndiye mvamizi wa eneo lao na si wananchi maana hata kijiji hakimtambui kwa maana hajawahi kufika kwao.

Nae Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Mvomero, Majaliwa Jaffari alisema watalishughulikia suala hilo haraka na hasa baada ya kufika eneo la tukio na kukiri kuna mapungufu katika ramani waliyonayo.

Agosti 23, mwaka huu wananchi hao waliitaka serikali kuingilia kati mgogoro huo haraka kabla ya machafuko kutokea wakati wakiwa katika mkutano wa hadhara uliokuwa uhudhuriwe na Mkurugenzi wa Wilaya na Maofisa wa Ardhi. Habari na Picha:Mroki Mroki

Saturday, August 27, 2011

Mama Salma Kikwete Aendesha Harambee Ya Kuchangisha Fedha Kwaajili Ya Tamasha La MOWE



Mwenyekiti wa Taasisi wa WAMA pia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na Wajasiriamali Aug 26,2011 jinini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la Wajasiriamali (MOWE) 2011 litalofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo mwaka huu Taasisi ya WAMA ndio mratibu wa Tamasha hilo.Jumla ya zaidi milioni 55 zimechangwa katika hafla hiyo na kauli mbiu ya mwka huu ya MOWE ( MIAKA 50 WANAWAKE WAJASIRIAMALI TUNAWEZA-TUTUMIE FURSA),(kulia ni Mwenyekiti wa MOWE Tanzania Elihaika Mrema,na (kushoto) ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Consolata I.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Alexio Musindo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la wajasiriamali (MOWE) yaani Month of Women Enterprenuers,
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akipokea vitabu kutoka kwa muwakililishi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania Gloria Kavishe(kulia) katika hafla ya Uzinduzi wa uchangiaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la Wajasiriamali (MOWE) August 26,2011, Vitabu hivyo vimekabidhiwa kwaajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule ya mfano ya watoto yatima WAMANAKAYAMA iliopo Rufiji mkoa wa Pwani,
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akipokea hundi ya shilingi milioni tano (5m/-) kutoka kwa Mwakilishi wa Bank ya CRDB (kulia)kwaajili ya kuchangia tamasha la wajasiriamali wanawake (MOWE) 2011 , (aug 26,2011)) jijini Dar es Salaam, Zaidi ya shiligi 55 milioni zimechangwa.(55,368,500/)
Baadhi ya Wanawake wajasiriamali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Slama Kikwete (Aug 26,2011) katika hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la wajasiriamali (MOWE) jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya MOWE na vbaadhi ya viongozi wa meza kuu akiwepo Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete.
Picha na Mwanakombo Juma-MAELEZO

Thursday, August 25, 2011

MAMBO YA STEPS HAYA !

Kampuni ya Steps entertainment na Kanumba the great films kwa pamoja, leo hii inasherehesha tukio la kihistoria katika tasnia ya filamu Tanzania. Tukio lenyewe ni kuhusu utolewaji wa filamu ya kwanza iliyoigizwa kwa ushirikiano kati ya wasanii nguli barani Afrika.
Ramsey Tonkubo Nouah wa Nigeria na Steven Kanumba wa Tanzania wameshirikiana na kufanya filamu bomba iitwayo “Devil’s Kingdom” ambayo itakuwa sokoni kesho ijumaa nchi nzima. “Jamani hatuko hapa kusherehekea hilo tu, bali tuko hapa pia kuwapa hamasa wasanii wengine hapa nchini hasa wachanga (Under-ground) kwamba Steps imejizatiti katika kuinua vipaji vya wasanii wachanga na aliyepewa jukumu la kuongoza filamu za Steps zitakazoshirikisha wasanii wapya kila mwezi ni director Selles Mapunda ambaye amepangiwa kutengeneza filamu 12 kuanzia leo mpaka mwezi kama huu mwakani akishirikisha pia wasanii nguli hapa nchini akiwemo Steven Kanumba, Ray, JB na wengineo”.
Alisema hayo Selles Mapunda ambaye pia ni Afisa Mahusiano ya Jamii katika kampuni ya Steps Entertainment. (Community Relation Officer).
Huu ni mwanzo wa safari ya Steps kuhakikisha kwamba Tasnia ya filamu Tanzania inakua kimataifa, il-hali mafanikio yake yanasaidia pia jamii na hasa wasiojiweza na watoto.
“Mungu aibariki hii tasnia” hayo pia ni moja ya maneno ya mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Steps Jairaj Domodoran....

Mhe. Mizengo Pinda Akijadilina na Edward Lowassa


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kushoto),akijadiliana jambo na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa Bungeni Mjini Dodoma jana.

Dewji; " Mangumbaru Wa Siasa Wananichefua!"


* Apeleka Singida mradi wa maji wa bil 20/-

Na Mwandishi Wetu


MBUNGE wa Singida Mjini, Mohammed Dewji amesema mangumbaru (watu wenye machachari, matata na fujo) wa siasa wanamchafua, kwa lengo la kuchukua kiti chake cha ubunge.


Dewji, maarufu kwa jina la Mo, ametoa kauli hiyo wakati akifanuzi tuhuma zilizotolewa na baadhi ya watu waliodai ni wakazi wa Singida, walioda eti kwamba hajafanya chochote cha maendeleo katika jimbo lake tangu achaguliwe kuwa mbunge.


Tuhuma na malalamiko hayo yaliyotolewa na baadhi ya watu waliodai ni wananchi wa Singida kupitia mtandao wa Facebook, wakati wa kubadilishana mawazo na mbunge huyo.


Pia Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) aliwataka wana-Singida kuungana na Watanzania wengine kufanya maandamano kudai ahadi ya maisha bora kwa wote kama ilivyoahidiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyoko madarakani.


Lema akiwa na wabunge wenzake, Chiku Abwao na Regia Mtema (Chadema - Viti Maalumu), alisema hayo wiki hii mjini Singida kwenye mkutano wa hadhara, huku akidai umefika wakati kwa wananchi wa Mkoa wa Singida ambao ni ngome ya CCM, kukiondoa chama hicho madarakani.


Katika michango yao kwenye Facebook, wananchi hao walioruhusiwa kutoa maoni na dukuduku zao kwa Dewji, walidai kutoona maendeleo yoyote katika jimbo hilo kwa madai kwamba wananchi wa Singida wamekuwa wakiteseka na maisha kwa kukosa maji, ajira na masuala ya maendeleo.


Katika ufafanuzi wake kuhusu malalamiko hayo, Dewji alisema tangu kuchaguliwa kwake amekuwa mstari wa mbele kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwenye maeneo ya kero za maji.


Dewji alisema amefanikisha uchimbaji wa visima virefu zaidi ya 21 kwenye kata za Unyambwa, Mungu Maji, Unyamikumbi, Mwankoko, Mtamaa, Mandewa na Mtipa pamoja na baadhi ya kata za Mjini kama Kindai, Mitunduruni na Utemini.


Dewji pia aliongeza kuwa bado anaendelea na jitihada za kukabiliana na tatizo hilo kwa kuibana Serikali itekeleze mradi mkubwa wa Benki ya Dunia wa kuchimba visima 10 jimboni na anaendelea kuibana Serikali ifanye haraka kumalizia mradi mkubwa mwingine wa maji unaofadhiliwa na Benki ya BADEA na OPEC.


"Mradi huo ukikamilika ndio utakuwa ufumbuzi wa tatizo la maji Manispaa ya Singida... Mradi huu utabadilisha miundombinu yote ya maji safi ndani ya manispaa yetu. Unatarajia kukamilika mwaka 2013 na utagharimu takriban sh. bilioni 20," alisema Dewji.


Kuhusu ajira, Dewji alieleza kuwa amekuwa mstari wa mbele kutoa Ajira kwa vijana kupitia kampuni yake ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL) sambamba na kampuni nyingine mbalimbali.


Alifafanua zaidi kuwa yuko mbioni kuwekeza katika jimbo lake kwa kufungua kiwanda kitakachotoa fursa zaidi kwa vijana na wakazi wa Singida kujipatia maendeleo na ajira, na kwamba kwa sasa anaendelea kuwasiliana na wataalamu mbalimbali wa uwekezaji ili kuona kama kuna fursa za kuwekeza katika manispaa ya hiyo.


Alipongeza kupokelewa kwa mwito wa kuhamasisha michezo katika jimbo lake na kusisitiza kuwa ataendelea kunyanyua na kuibua vipaji kupitia mashindano yake yajulikanayo kama Mohammed Dewji Cup yakiwa na takriban miaka saba na yamekuwa na mafanikio makubwa kwa vijana wazaliwa wa Singida.


"Kuhusiana na suala la ujenzi wa Uwanja wa Namfua, nilishaanza ukarabati katika eneo la jukwaa kuu, wananchi ni mashahidi... kama wanaufahamu uwanja ulivyokuwa mwanzo na wakati wa mashindano ya riadha kitaifa, nilikarabati eneo la kukimbilia wanariadha.


"... Bado nitaendelea kukarabati kwa awamu mpaka tutakapoukamilisha. Ukumbuke ahadi hii haikuwa yangu peke yangu. Lakini nimeshanunua nyasi za bandia ambazo zimenigharimu sh. milioni 250... Natarajia kuziweka hizo nyasi mwaka 2012/2013," alisema Dewji.

Wednesday, August 24, 2011

AU kuchangisha pesa za janga la njaa

Njaa Somalia
Njaa Somalia
Viongozi wa Afrika wanakutana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, kuchangisha pesa ili kukabiliana na mzozo wa kibinadamu unaokabili eneo la pembe ya Afrika.
Mkutano wa leo ulitarajiwa kufanyika wiki mbili zilizopita, lakini ukaahirishwa ili kuupa Muungano wa Afrika muda zaidi kuandaa mkutano huo.
Dola millioni moja na nusu zaidi zinahitajika kukabiliana na janga la njaa, linaloathiri nchi tano barani Afrika. Somalia ambako mzozo wa kisiasa bado unaendelea ndiyo iliyoathirika zaidi .
Mkutano huu wa kuchangisha fedha ni wa kwanza wa aina yake kufanywa na Muungano wa Afrika.
Mwenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika, Jean Ping, amesema juhudi za muungano huo hazitoshi na madhumuni ya mkutano huu wa siku moja ni kuchangisha dola billioni moja na nusu kufadhili janga hilo.
Nchi kadhaa za Afrika tayari zimetoa michango yao katika juhudi hizo za kibinadamu, lakini muungano huo umeshutumiwa kwa kuchelewa kushughulikia janga hilo kwa haraka.
Hata hivyo, Muungano huo umejitetea na kusema ulihitaji muda zaidi kushirikiana na wanachama wake na kuandaa mkutano.
Waandalizi wa mkutano huu wanasema mkutano wenyewe hautachangisha pesa pekee , lakini pia viongozi watajadili suluhu za kudumu za kukabiliana na majanga ya kibinadamu barani Afrika.Chanzo ni bbckiswahili.com

Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa,Mbunge wa Hai,Freeman Mbowe,Mbunge wa Bumbuli January Makamba,Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe,Mbunge wa Vunjo Augustine Lyatonga Mrema washiriki Maziko Ya Marehemu Mussa


Waziri Mstaafu, Edward Lowassa,  akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa maziko yaliyofanyika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya kati Unguja leo Agosti 24.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa maziko yaliyofanyika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya kati Unguja leo Agosti 24.
Mwenyekiti wa Makati ya Bunge ya kudumu ya Heshabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Hamis Silima, wakati wa maziko yaliyofanyika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya kati Unguja leo Agosti 24.
Rais wa Zanzibar,Dkt.  Ali Mohamed Shein, Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Mohammed Gharib Bilal,Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim Seif na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa,Mbunge wa Bumbuli na Mwenyekiti wa Kamati ya nishati na madini January Makambawakiwa katika shughuli ya mazikonya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, marehemu Mussa Silima. Maziko hayo yamefanyika leo Agosti 24 katika Kijiji cha Kiboje Wilaya ya Kati Unguja.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais

Jeshi La Polisi Zanzibar Lakamata Magudia Ya Dagaa Yaliyojazwa Pembe Za Tembo Written by haki | // 0 comments HIVI ndivyo ilivyokuwa jinsi ilivyohifadhiwa Mkuu wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar SP Martin Lissu akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio bandarini Zanzibar wakati wa zoezi likiendelea. Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar ACP. Muhud Mshihiri akizungumza na wakala wa kusafirisha mizingi na msimamizi wa mzingo huo, wakati wa zoezi la kuendelea kupekuwa magunia ya Dagaa ikiwa ndani yake mmeweka Pembe za Tembo, kulia Kamanda wa Polisi Marine Zanzibar SP Martin Lissu. MMOJA ya Konteni lilokuwa likisubiri kusafirishwa na kago ya magunia ya Dagaa na kuchanganywa na Pembe za Tembo likiwa katika upekuzi baada ya kugundulika kuwa na Nyara za Serikali zikitaka kusafirishwa nje ya Nchi. HIVI ndivyo ilivyokuwa kufunguwa kila gunia kutowa kisicho husika katika magunia ya Dagaa inayosemekana yakitokea Mwanza na kusafirishwa nje kupitia bandari ya Zanzibar. KIPUSA kikitolewa katika magunia ya dagaa wakati wa zoezi hilo likiendelea katika bandari ya Zanzibar. KIPUSA kikitolewa katika magunia ya dagaa wakati wa zoezi hilo likiendelea katika bandari ya Zanzibar.Picha Zote na Mdau Othman Maulid -- Na Mwandishi wa MAELEZO-Zanzibar Polisi Visiwani Zanzibar wamekamata Shehena kubwa ya Pembe za ndovu katika Bandari ya Malindi Visiwani hapa. Hii ni Shehena kubwa ya kwanza kukamatwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba ambapo Polisi walifanikiwa kuigundua baada ya taarifa za Kiintelijensia zilizofanyiwa kazi kitaalam. Shehena hiyo ya Vipusa ilikuwa imepakiwa katika makontena mawili huku kukiwa na shehena ya samaki aina ya dagaa wa maji baridi. Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na Mamlaka husika, zinadai kuwa Shehena hiyo ya Pembe za Ndovu ilikuwa ikipelekwa nchini Malaysia.Hadi saa 1:00 usiku Polisi walikuwa wakiendelea na kazi ya upakuaji na upekuzi zaidi katika eneo la Bandari ambapo kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi Bandarini,Martin Lissu watu wawili wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi. Watu waliokamatwa ni pamoja na Wakala wa mizigo ambaye Polisi wamesema ni mapema mno kumtaja kwa sababu za kiupelelezi.

 HIVI ndivyo ilivyokuwa jinsi ilivyohifadhiwa
 Mkuu wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar SP Martin Lissu akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio bandarini Zanzibar wakati wa zoezi likiendelea.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar ACP. Muhud Mshihiri akizungumza na wakala wa kusafirisha mizingi na msimamizi wa mzingo huo, wakati wa zoezi la kuendelea kupekuwa magunia ya Dagaa ikiwa ndani yake mmeweka Pembe za Tembo, kulia Kamanda wa Polisi Marine Zanzibar SP Martin Lissu.  
 MMOJA ya Konteni lilokuwa likisubiri kusafirishwa na kago ya magunia ya Dagaa na kuchanganywa na Pembe za Tembo likiwa katika upekuzi baada ya kugundulika kuwa na Nyara za Serikali zikitaka kusafirishwa nje ya Nchi. 
 HIVI ndivyo ilivyokuwa kufunguwa kila gunia kutowa kisicho husika katika magunia ya Dagaa inayosemekana yakitokea Mwanza na kusafirishwa nje kupitia bandari ya Zanzibar.
 KIPUSA kikitolewa katika magunia ya dagaa wakati wa zoezi hilo likiendelea katika bandari ya Zanzibar. 
KIPUSA kikitolewa katika magunia ya dagaa wakati wa zoezi hilo likiendelea katika bandari ya Zanzibar.Picha Zote na Mdau Othman Maulid 
--
Na Mwandishi wa MAELEZO-Zanzibar
Polisi Visiwani Zanzibar wamekamata Shehena kubwa ya Pembe za ndovu katika Bandari ya Malindi Visiwani hapa.

Hii ni Shehena kubwa ya kwanza kukamatwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba ambapo Polisi walifanikiwa kuigundua baada ya taarifa za Kiintelijensia zilizofanyiwa kazi kitaalam.
Shehena hiyo ya Vipusa ilikuwa imepakiwa katika makontena mawili huku kukiwa na shehena ya samaki aina ya dagaa wa maji baridi.

Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na Mamlaka husika, zinadai kuwa Shehena hiyo ya Pembe za Ndovu ilikuwa ikipelekwa nchini Malaysia.Hadi saa 1:00 usiku Polisi walikuwa wakiendelea na kazi ya upakuaji na upekuzi zaidi katika eneo la Bandari ambapo kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi Bandarini,Martin Lissu watu wawili wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi.

Watu waliokamatwa ni pamoja na Wakala wa mizigo ambaye Polisi wamesema ni mapema mno kumtaja kwa sababu za kiupelelezi.

 HIVI ndivyo ilivyokuwa jinsi ilivyohifadhiwa
 Mkuu wa Kikosi cha Polisi Bandarini Zanzibar SP Martin Lissu akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio bandarini Zanzibar wakati wa zoezi likiendelea.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar ACP. Muhud Mshihiri akizungumza na wakala wa kusafirisha mizingi na msimamizi wa mzingo huo, wakati wa zoezi la kuendelea kupekuwa magunia ya Dagaa ikiwa ndani yake mmeweka Pembe za Tembo, kulia Kamanda wa Polisi Marine Zanzibar SP Martin Lissu.  
 MMOJA ya Konteni lilokuwa likisubiri kusafirishwa na kago ya magunia ya Dagaa na kuchanganywa na Pembe za Tembo likiwa katika upekuzi baada ya kugundulika kuwa na Nyara za Serikali zikitaka kusafirishwa nje ya Nchi. 
 HIVI ndivyo ilivyokuwa kufunguwa kila gunia kutowa kisicho husika katika magunia ya Dagaa inayosemekana yakitokea Mwanza na kusafirishwa nje kupitia bandari ya Zanzibar.
 KIPUSA kikitolewa katika magunia ya dagaa wakati wa zoezi hilo likiendelea katika bandari ya Zanzibar. 
KIPUSA kikitolewa katika magunia ya dagaa wakati wa zoezi hilo likiendelea katika bandari ya Zanzibar.Picha Zote na Mdau Othman Maulid 
--
Na Mwandishi wa MAELEZO-Zanzibar
Polisi Visiwani Zanzibar wamekamata Shehena kubwa ya Pembe za ndovu katika Bandari ya Malindi Visiwani hapa.

Hii ni Shehena kubwa ya kwanza kukamatwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba ambapo Polisi walifanikiwa kuigundua baada ya taarifa za Kiintelijensia zilizofanyiwa kazi kitaalam.
Shehena hiyo ya Vipusa ilikuwa imepakiwa katika makontena mawili huku kukiwa na shehena ya samaki aina ya dagaa wa maji baridi.

Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na Mamlaka husika, zinadai kuwa Shehena hiyo ya Pembe za Ndovu ilikuwa ikipelekwa nchini Malaysia.Hadi saa 1:00 usiku Polisi walikuwa wakiendelea na kazi ya upakuaji na upekuzi zaidi katika eneo la Bandari ambapo kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi Bandarini,Martin Lissu watu wawili wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi.

Watu waliokamatwa ni pamoja na Wakala wa mizigo ambaye Polisi wamesema ni mapema mno kumtaja kwa sababu za kiupelelezi.

Tuesday, August 23, 2011

MBUNGE SILIMA AFARIKI KUFUATIA AJALI YA GARI ILIYOTANGULIA KUMUUA MKEWE

 

Marehemu Musa Hamisi Silima

Marehemu mbunge Silima


Mbunge mteule kutoka Baraza la Wawakiilishi Zanzibar,Mussa Khamis Silima ambaye alipata ajali majuzi katika eneo la Nzuguni Dodoma akiwa katika kitanda maalum cha kubebea wagonjwa, Hospitali ya Muhimbili baada ya kushushwa kwenye gari akitokea Dodoma alikopata ajali ambapo mkewe Bi Mwanakheir Fahari alifariki Dunia

Gari la Marehemu Mbunge Silima
---
Mbunge Mussa Hamisi Silima, aliyejeruhiwa baada ya kupata ajali jana mjini hapa,
amefariki dunia Silima alifariki dunia leo saa tano asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ambako alihamishiwa na kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu
zaidi.


Taarifa za kifo cha Silima zilitangazwa jana saa 5.50 asubuhi na Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati wabunge wakiendelea kuchangia makadirio ya mapato na
matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2011/2012"Waheshimiwa wabunge, kama mtakumbuka jana niliwatangazia kwamba, mheshimiwa Mussa Hamisi Silima, alipata ajali mbaya eneo la Nzuguni, ambapo mke wake, Mwanaheri Twalib alifariki dunia hapo hapo.


"Aidha niliwaarifu kuwa, mheshimiwa Silima na dereva wake walipata majeraha makubwa na wamepelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi. Leo asubuhi kabla ya maswali,nimetoa taarifa kwenu kwamba nimeongea na mheshimiwa Silima akiwa anaendelea kupata matibabu. Ni kweli nimeongea naye.


"Kwa masikitiko makubwa, nawatangazieni kuwa, nimepokea taarifa kutoka kwa katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii kwamba, mheshimiwa Mussa Hamisi Silima amefariki dunia muda mfupi tu uliopita"Kwa mujibu wa kanuni ya 149 ya kanuni za bunge, toleo la mwaka 2007, ninaahirisha shughuli za bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi," alisema.
Kufuatia msiba huo, Spika Anne aliwataka wabunge wasimame kwa dakika moja kwa heshima ya mbunge huyo.


Spika alisema kwa kipindi cha siku tatu, familia ya Silima imekumbwa na matatizo makubwa, kufuatia kutanguliwa na msiba wa kaka wa mkewe kabla ya mkewe naye kufariki dunia.
Katika ajali iliyotokea jana eneo la Nzuguni, mke wa mbunge huyo, Mwanaheri
alikufa papo hapo eneo la ajali wakati dereva wake, Chizali Sembonga, aliyekuwa
akiendesha gari aina ya Toyota Corolla, lenye namba za usajili T 509 AGC
alijeruhuwa.


Silima na mkewe walipatwa na ajali hiyo walipokuwa wakirejea Dodoma. Mbunge
huyo alikuwa amekwenda Zanzibar kuhudhuria maziko ya kaka wa mkewe,Mwanaheri.Mbunge huyo na dereva wake walisafirishwa kwa ndege juzi kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Mwili wa Mwanaheri ulizikwa juzi alasiri.

VodacomYatoa Fursa Kwa Watanzania Kuwapigia Kura Warembo

 


Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetoa fursa kwa Watanzania kuweza kupiga kura na kuchagua mrembo anaevutia zaidi kati ya warembo 30 wanaoshiriki katika shindano la kumsaka Vodacom Miss Tanzania 2011.
Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Bw. George Rwehumbiza alisema ili kupiga kura Watanzania watatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno MREMBO ukifuatiwa na namba ya mshiriki kwenda 15550 ambapo gharama kwa kila ujumbe ni shilingi 150 tu .
Aidha Bw, Rwehumbiza aliongeza kuwa kila ujumbe mfupi utakaotumwa utampatia Mtanzania pointi 10 ambapo wateja 20 watakaobahatika kuwa na pointi nyingi zaidi kila mmoja atajipatia TIKETI mbili za VIP zitakazomwezesha kwenda kushuhudia fainali ya Vodacom Miss Tanzania 2011 itakayofanyika tarehe 10 mwezi septemba katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dares salaam.
Pia kwa wale watakaohitaji kutoa maoni au mitazamo yao mbalimbali kuhusu Vodacom Miss Tanzania watapata fursa ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye neno MREMBO ukifuatiwa na maoni kwenda namba 15550.
Akisisitiza hili Bw. Rwehumbiza alisema ili kuwafahamu warembo wanaoshindania taji la Vodacom Miss Tanzania 2011 Watanzania wote wanaweza kuangalia kituo cha STAR TV leo kuanzia muda wa saa moja jioni pamoja na CLOUDS TV muda wa saa tatu usiku kila siku pia soma magazeti ya Mtanzania, The African,Dimba,Rai na Bingwa.

Monday, August 22, 2011

Mwanawe Gaddafi aapa kupambana na waasi

Saif al-Islam
Mwanawe Gaddafi Saif al-Islam
Mtoto wa kiume wa Kanali Muammar Gaddafi, Saif al-Islam, ambaye awali waasi walidai kuwa wamemkamata, amejitokeza katika hoteli moja inayoshikiliwa na wafuasi wa Kanali Gaddafi.
Mwandishi wa BBC Matthew Price amezungumza na Saif al-islam na kusema kuwa anaonekana kuwa mchangamfu na shauku kuu.
Saif al-Islam amesema waasi wameingia kwenye ''mtego'' mjini Tripoli na kwamba wanajeshi wanaomuunga mkoni Kanali Gaddafi walikuwa ''wamevunja uti wa mgogo wa waasi hao''.
Waasi wanaopigana kuudhibiti mji mkuu wa LibyaTripoli , wamerudishwa nyuma na wanajeshi wanaomuunga mkono Kanali Muammar Gaddafi.
Lakini wakati mapigano yanapoendelea katika maeneo mbalimbali ya mji, msafara wa waasi kutoka mashariki mwa nchi ulirudishwa nyuma.

Bado hajulikani alipo Kanali Gaddafi.

Jumapili iliyopita waasi walidai kuwa walikuwa wamemkamata Saif al-Islam, pamoja na familia yake.
Hata hivyo, bado Kanali Gaddafi hajulikani alipo. Nyumba yake inalindwa na wapiganaji wanaomtii.
Waasi hao walioingia mjini Tripoli jumamosi iliyopita walikaribishwa watu waliokuwa wakisheherekea katika bustani ya Green Square wakati walipowasili siku ya jumapili.
Waasi hao wamesema kuwa wameweka vizuizi katika sehemu mbalimbali za mji lakini wanakabiliwa na upinzani mkali katika baadhi ya maeneo.
Kamanda wa waasi amesema wanadhibiti asilimia 90 ya mji wa Tripoli.
Kiongozi wa Baraza la Mpito la kitaifa (NTC), Mustafa Abdel Jalil, amesema wakati wa ushindi halisi utakuwa pale watakapo mkamata Kanali Gaddafi.

Rais Obama apongeza watu wa Libya.

Rais Barrack Obama amewapongeza watu wa Libya kwa kile alichokitaja kama ''kujitolea mhanga kusipokuwa kwa kawaida''. Obama amesema watu wa Libya wanakaribia kupata kile wanachohitaji.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Ban Ki-Moon naye amewakumbusha wanachama wa Umoja huo kuwa, wanajukumu la kuheshimu mahakama ya kimataifa ya jinai, ambayo imetoa hati za kuwakamata Kanali Gaddafi, mtoto wake wa kiume Saif al Islam na mkuu wake wa idara ya ujasusi.
Baadhi ya viongozi wa waasi wanasema afadhali wafunguliwe mashtaka nchini Libya na sio katika mahakama ya kimataifa ya ICC, mjini The Hague.Chanzo ni bbc

Chuo Cha Ualimu St. Augustine Tawi la Mtwara Walipoamuaga Mama Salma Kikwete


Picha ya pamoja Kati ya Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete(mwenye baibu) na walimu wanafunzi i kutoka chuo cha ualimu STAugustine, tawi la Mtwara waliokwenda kumuaga ofisini kwake Aug,20,2011 baada ya kumaliza mafunzo ya ualimu kwa vitendo kwenye shule ya mfano ya watoto yatima WAMA-NAKAYAMA inayofadhiliwa na Taasisi ya WAMA huko Rufiji mkoa wa Pwani.Mstari wa nyuma alievaa T-Shirt ya mistari ni Katibu wa WAMA Daud Nasib
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia)akiwakabidhi zawadi baadhi ya walimu wanafunzi saba kutoka Tawi la Chuo cha Ualimu St. Augustine tawi la Mtwara Aug 20,211 walipokwenda kumuaga ofisini kwake baada ya kumaliza mafunzo ya ualimu kwa vitendo katika shule ya mfano ya watoto yatima WAMA-NAKAYAMA Mkoa wa Pwani,.(katikati ni Mwalimu mwanafunzi Kaiza Magoa na (kushoto) Kiongozi wao Victoria John.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete(kulia alievaa baibui)akiongea Ofisini kwake Aug,20-2011 na walimu wanafunzi kutoka chuo cha Ualimu St. Augustine tawi la Mtwara waliomaliza mafunzo kwa vitendo katika shule ya mfano ya watoto yatima WAMA -NAKAYAMA iliopo chini ya Taasisi ya WAMA. huko Rufiji mkoani Pwani.Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

Sunday, August 21, 2011

Gaddafi Maji Ya Shingo; Waasi Wathibiti Mji Wa Tripol

Picha za televisheni zinaonyesha waasi katika uwanja wa Green Square katika mji mkuu, huku makundi ya watu wenye furaha wakisheherekea kuwasili kwa waasi hao katika uwanja huo.
Inaripotiwa waasi wamemkamata mwanawe Gaddafi Saif al-Islam, huku kiongozi mwenyewe akiahidi kuwa ataendelea kupigana.
Mwendesha mashtaka wa mahakama ya uhalifu wa kivita, Luis Moreno Ocampo amethibitisha Saif al-Islam, mwanawe Gaddafi, na ambaye alitarajiwa kumridhi babake amekamatwa.
Mwanawe wa kifungua mimba Mohammed Al Gaddafi naye amejisalimisha kwa waasi na anazuiliwa ndani ya makaazi moja mjini Tripoli.
Serikali ya Libya imesema takriban wanajeshi elfu 65 watiifu kwa kanali Gaddafi wamebakia mjini Tripoli lakini ni wachache tu walioonekana wakati waasi walipokuwa wakielekea kuuteka mji huo.
Mapigano yameripotiwa katika maeneo mengine ya mji. Mwandishi wa BBC mjini Tripoli amesema waasi wanajaribu kushika udhibiti wa jengo ambalo waandishi wa habari wako.
Inaaminika kuwa bado Kanali Gaddafi ana maelfu ya wafuasi waliojihami, japo ripoti zinaashiria kuwa idadi kubwa wamejisalimisha kwa waasi.
Msemaji wa serikali ya Libya , Moussa Ibrahim, amesema takriban watu 1300 wameuwawa mjini humo.
Awali Kanali Gaddafi aliwataka raia kujitokeza na kuukomboa mji wa Tripoli. '' Jitokezeni, jitokezeni niko nanyi. Msirudi nyuma. Tutapigana hadi kuikomboa nchi yetu kuzuia uthibiti. Msiwakubalie wanyakuzi kuiteka nchi yetu, nitapigana pamoja nayi kama nilivyoahidi'', Alisema Muammar Gaddafi.BBC

Saturday, August 20, 2011

SPORAH SHOW WINS THE FACE OF 2012 SPECIAL RECOGNITION AWARDS ON WORLD HUMANITARIAN DAY..!


 Special thanks goes to all my entire team who work tirelessly on this production.

Kitabu cha Mwongozo wa Katiba Chazinduliwa Jijini Dar es Salaam



Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, akikata utepe kauashiria kuzindua chapisho Mwongozo wa Katiba kwa Raia, jijini Dar es Salaam jana. Uzinduzi huo ulifanyiaka katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo mbele katika mkutano na waandishiwa habari. Mwingine ni Hebron Mwakagenda, Mwenyekiti mwenza wa Policy Forum, waandaaji wa chapisho hilo.