Monday, August 22, 2011

Chuo Cha Ualimu St. Augustine Tawi la Mtwara Walipoamuaga Mama Salma Kikwete


Picha ya pamoja Kati ya Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete(mwenye baibu) na walimu wanafunzi i kutoka chuo cha ualimu STAugustine, tawi la Mtwara waliokwenda kumuaga ofisini kwake Aug,20,2011 baada ya kumaliza mafunzo ya ualimu kwa vitendo kwenye shule ya mfano ya watoto yatima WAMA-NAKAYAMA inayofadhiliwa na Taasisi ya WAMA huko Rufiji mkoa wa Pwani.Mstari wa nyuma alievaa T-Shirt ya mistari ni Katibu wa WAMA Daud Nasib
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia)akiwakabidhi zawadi baadhi ya walimu wanafunzi saba kutoka Tawi la Chuo cha Ualimu St. Augustine tawi la Mtwara Aug 20,211 walipokwenda kumuaga ofisini kwake baada ya kumaliza mafunzo ya ualimu kwa vitendo katika shule ya mfano ya watoto yatima WAMA-NAKAYAMA Mkoa wa Pwani,.(katikati ni Mwalimu mwanafunzi Kaiza Magoa na (kushoto) Kiongozi wao Victoria John.
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete(kulia alievaa baibui)akiongea Ofisini kwake Aug,20-2011 na walimu wanafunzi kutoka chuo cha Ualimu St. Augustine tawi la Mtwara waliomaliza mafunzo kwa vitendo katika shule ya mfano ya watoto yatima WAMA -NAKAYAMA iliopo chini ya Taasisi ya WAMA. huko Rufiji mkoani Pwani.Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

No comments:

Post a Comment