Sunday, August 7, 2011

China kuimarisha uhusiano na Sudan Kusini


ramani ya Sudan na Sudan Kusini
Waziri wa mambo ya nje wa China Yang Jiechi, anaanza ziara rasmi inayotajwa kuwa na umuhimu mkubwa mjini Khartoum.
Baadaye kiongozi huyo ataelekea mjini Juba kukutana na viongozi wa taifa jipya la Sudan Kusini. China imekuwa mshirika wa karibu na utawala wa Khartoum tangu kuanza kuuziwa mafuta yake miaka ya tisini. Lakini taswira imebadilika na Sudan Kusini imesalia na raslimali nyingi ya mafuta.
Siyo kawaida kwa waziri wa mambo ya nje kutoka moja ya nchi tajiri duniani kufanya ziara rasmi mjini Khartoum.
Waziri wa mambo ya nje wa China Yang Jiechi anafanya kikao maalum na mwenzake wa Sudan Ali Khati hii leo katika kile kiemetajwa kama mazungumo ya uhusiano kati ya pande mbili.
Hata hivyo uhusiano kati ya Sudan na nchi mpya ya Sudan Kusini hususan masuala ya usalama, mafuta na uraia yatajitokeza kwenye kikao hiki. Bw. Jiechi aidha anatarajiwa kukutana na rais Omar Al Bashir baadaye jioni.
Kiongozi huyo kwa sasa yuko nchini Chad ambapo anahudhuria kuapishwa kwa rais Idriss Deby kwa muhuma mwingine. Hapo kesho Jumanne, waziri wa mambo ya nje atafanya ziara mjini Juba ikiwa ni ziara ya kwanza ya afisa wa juu kutoka China tangu Sudan Kusini kujitangazia huru wake mwezi jana.
China imeonekana kuimarisha taswira yake barani Afrika katika kile kimatajwa kama hatua ya kupata mali ghafi ya bara hili. Sudan Kusini imejitenga na kubakia na raslimali kubwa ya mafuta. Wengi wanahoji ikiwa China italegeza uhusiano wake na utawala wa Khartoum. China imekuwa ikiitetea Sudan katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Aidha taifa hilo lilisimama na rais Bashir pale mahakama ya kimataifa ya Jinai ilipotoa kibali cha kumkamata rais Bashir kwa mauaji ya halaiki katika jimbo la Darfur. Siku kadhaa kabla ya uhuru wa Sudan Kusini rais Bashir alialikwa mjini Beijing katika kile kilitajwa kama hatua ya China kuihakikisha Sudan kwamba ilikuwa mshirika wake wa karibu.
Lakini pia China inanuia kuimarisha uhusiano na Sudan Kusini. Kwa sasa imeanzisha miradi nane. Mmoja wa miradi hiyo raia wa Sudan Kusini wanapata maarifa ya uzalishaji kwenye visima vya mafuta.Kuna pia hoteli kadhaa za kichina mjini Juba.
China inanuia kusaidia Sudan na Sudan Kusini kuimarisha uhusiano wao ikikisiwa kwamba mafuta yanayouziwa China na Sudan Kusini husafirishwa na mbomba kupitia Sudan.
Hata hivyo majirani hawa wanatarajiwa kuendelea kuwa na uhusiano ulioyumba.
Ziara ya Yang Jiechi huenda ikaashirikia ikiwa China itaendelea kuimarisha uhusiano wake na rafiki wa zamani Khartoum au itasimama na rafiki mpya na tajiri wa mafuta aliyeko Juba.Chanzo www.bbckiswahili

No comments:

Post a Comment