Wednesday, May 16, 2012

BAVICHA Wamsulubu Shibuda

 


TAMKO LA BAVICHA KUHUSIANA NA KAULI ILIYOTOLEWA NA MHE.JOHN SHIBUDA

MBUNGE WA MASWA MASHARIKI.

BAVICHA imepokea kwa mshituko mkubwa kauli ya ndugu Shibuda kuwa yeye

atagombea Urais na Meneja wake wa Kampeni atakuwa Mwenyekiti wa CCM ndugu

Jakaya Kikwete, na alitoa kauli hiyo kwenye kikao cha NEC ya CCM.

MAMBO YAFUATAYO YEMETUSHTUA;

1. Katoa Kauli hiyo kwenye kikao cha NEC ya CCM

2. Meneja wa kampeni zake amemtangaza kuwa ni Mwenyekiti wa CCM taifa

Jakaya Kikwete

3. Amesema kuwa hakuna chama kingine chenye uwezo wa kuiongoza nchi kwa

sasa

4. Alitoa tamko hilo kwa niaba ya APRM .

Mambo hayo manne ndio yametushtua na kutufedhehesha sana sisi vijana wa

CHADEMA na ndio maana tumelazimika kutoa kauli kuhusiana na suala hili , na kauli

yetu ni kama ifuatavyo;

1. Kamwe BAVICHA hatutaruhusu mgombea Urais wa CHADEMA meneja wake

wa kampeni awe ni Mwenyekiti wa CCM hata siku moja kwani tunao watu wa

kutosha na wenye uwezo wa kutosha kuifanya kazi hiyo na hatuhitaji msaada

huo .

2. Kamwe hatutaruhusu mgombea urais wa CHADEMA awe anatangaza nia kwenye

vikiao vya CCM kwani hawana mamlaka ya kumteua mgombea wa CHADEMA

na kama Shibuda alikuwa halijui hilo anapaswa kulifahamu kuanzia sasa kuwa

vijana wa CHADEMA hatuchaguliwi mgombea na NEC ya CCM kwani CHADEMA

kuna vikao na taratibu zetu za kuteua wagombea.

3. Kusema kuwa hakuna chama kingine chenye uwezo wa kuongoza nchi ni

kutudhalilisha sisi vijana wa CHADEMA na watanzania wote ambao leo wanaiona

CHADEMA kama tumaini pekee la kuwakomboa, kauli hii tunaamini kama vijana

wa CHADEMA kuwa mamlaka za nidhamu hazitakaa kimya na kuiachia kauli ya

namna hii iachwe bila kutakiwa maelezo ya kina , tutaitisha kikao cha BARAZA

na tutaijadili kauli hii na kuwasilisha mapendekezo yetu kwenye vikao halali

vya chama .

4. Tunapenda kumwambia kuwa kama anaona kuwa yeye haendani na utamaduni

wa chama chetu na anakiona kuwa hakina uwezo wa kuongoza dola anafanya

nini kwenye chama ambacho anona kuwa hakiwezi kuongoza dola? Kwanini

atafute urais kwenye chama ambacho anaona hakiwezi kuongoza dola ?

anawatania watanzania? Ni heri akaenda kwenye hicho ambacho anaamini kuwa

kinaweza kuongoza dola , kwani lengo la chama chochote kile ni kuchukua dola

na sio vinginevyo.

5. Mwisho tunapenda kuwahakikishia vijana wote wa Tanzania na wananchi kwa

ujumla kuwa tayari CHADEMA kimejiandaa kikamilifu kuongoza dola na wasiwe

na hofu na maneno yaliyotamkwa na Mbunge huyu .

6. Natoa wito kwa Vijana wenzangu wote wa CHADEMA kuwa sasa tujiandae

kikamilifu katika kukabiliana na mtu yeyote yule ambaye ataonekana kuwa

kikwazo kwa chama chetu na wananchi kwa ujumla wake katika kuelekea

kuchukua dola 2015 .

Nawatakia kila la kheri katika ujenzi wa chama na tuendeleze operesheni ya ‘Vua

Gamba, Vaa Gwanda’ popote pale tulipo nchini.

Imetolewa leo Dar es Salaam, Mei 16, 2012 na;

John Heche

Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa.

No comments:

Post a Comment