Thursday, May 31, 2012
Wabunge wa Chadema Waangwa rasmi kwa kuangalia mechi ya kimataifa kati ya Brazil na Marekani
Baaada ya kazi kubwa ya kuzindua na kuimarisha tawi la chadema Washington Dc Maryland na Virginia,Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Mhe. Peter Msigwa na Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, Usiku wa Jana Jumatano Mei 30,2011 waagwa rasmi kwa kuangalia mpambano wa kimataifa kati ya US na Brazil ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini marekani
Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Peter Msigwa na Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, wakiwa na uwongozi wa tawi la Chadema Washington Dc Libe Mwangombe, wanne, Mjomba a.k.a Cosmas, Mzee wa swahilivilla Aboh Shatry wa pili kulia, pamoja na mashabiki wa US, wakiiunga mkono bendera ya taifa.
Idadi ya wapenzi waliohudhuria katika mpambano huo ni 67,656 wakiwemo Mhe. Nassari Joshua pamoja na Mhe, Peter Msigwa.
Wabunge wa chama cha Chadema wakipata flash ya pamoja na warembo wa Kibrazil ndani ya uwanja wa FedexField, uliopo Landover Maryland Nchini marekani.
Picha ya pamoja na viongozi wa juu wa Chadema kwenye mpambano wa US na Brazil Usiku wa kuamkia leo Alhamis Mei 31,2012 ndani ya ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini marekani
![]() |
Forward wa United States Landon Donovan, akipandisha majeshi juu huku alidhibitiwa na Brazil defender Marcelo wa Brazi katika mpambano wa kirafiki. |
Nabendera ya Taifa wakishangilia Bao la kwanza la Brazil lilifungwa kwa Penalti na mchezaji Neymar
Wachezaji wa Brazil wakilinda ngome yao kwa kuwadhibiti timu ya US kwenye mechi hiyo ya kirafiki ambapo timu ya Brazil waliweza kuwabamiza US bao 4-1 nyumbani kwao.
Wednesday, May 30, 2012
JK ampokea Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais Allasane Ouattara uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro jijini Arusha jana, akiwa ni mmoja wa wageni mashuhuri kuhudhuria mkutano wa AfDB. Picha na IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na mgeni wake Rais Allasane Ouattara uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro.
Wabunge Pamoja na Viongozi wa tawi la chadema Washington DC Watembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Baada ya kazi pevu ya uzinduzi wa tawi la Chadema jijini Washington Dc wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamtembelea rasmi Balozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar akipata picha ya pamoja na Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Msigwa ndani ya Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Wabunge wa Chadema Mhe. Peter Msigwa wapili kushoto, Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo Janja, (Watatu kulia), ofisa wa ubalozi Mhe. Peter Msigwa, Kaimu Balozi Mhe Lilian Munanka pamoja na viongozi wa tawi la Chadema Washington Dc wakipata picha ya pamoja na balozi Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar baada ya kumtembelea rasmi siku ya Jumanne Mei 29,2012 Washington Dc Nchini Marekani.
Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Peter Msigwa akipata picha ya pamoja na waTanzania waishio nchini Marekani, ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington Dc. (Picha na swahilivilla.blogspot.com)
Tuesday, May 29, 2012
HII NDIYO TAARIFA YA MARTIN SOSPETER BAADA YA KUJIUNGA NA BENDI YA MASHUJAA
Meneja mpya wa bendi ya Mashujaa Martin Sospeter akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotangaza kujiunga na bendi hiyo kwenye ukumbi wa Busness Kijitonyama asubuhi hii, kulia katika picha ni King Dodoo Kaimu Meneja wa bendi ya Mashujaa.
Bw. Martin Sospeter katikati akilalamikia shutuma zilizoelekezwa kwake na bendi ya African Stars wakati alipoongea na wanahabari asubuhi hii kwenye ukumbi wa Busness Kijitonyama, kulia ni Kaimu Meneja wa bendi hiyo King Dodoo na kushoto ni Rais wa Bendi ya Mashujaa Charles Baba.
Juzi usiku nilishangazwa na kauli ya mkurugenzi wangu wa Asha Baraka katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa amenifukuza kazi kutokana kuhujumu bendi ikiwemo kushawishi wanamuziki kujiunga na bendi ya Mashujaa
Kwa kweli kauli ile ilinisikitisha sana kutokana na ukweli kwamba Asha nilimchukulia kama zaidi ya dada kwani nilifanya naye kazi kwa miaka 14 iweje hii leo aje anitolee maneno ya kunichafua katika vyombo vya habari?
Mimi sijawahi kuhusika na mpango wowote wa wasanii wa Twanga kuhamia Mashujaa na wala sikuwa nafahamu mpango huo zaidi ya mwisho wa siku kusikia fununu za chinichini na mwishowe wasanii hao kutanghazwa kuhamia Mashujaa.
Leo napenda nitangaze rasmi kwamba nimeachana na African Stars na kujunga na Mashujaa Entertainment na tayari nimeshasaini mktaba wa kazi katika bendi hii.
“Nilipanga nifanye taratibu za kumuaga kutokana na kuwa nilikuwa nafanya kazi kwake bila ya mkataba lakini nimepata bendi hii ambayo tulikaa na kukubaliana mambo mbal;imbali.
Mbali na mkataba baadhi ya makubaliano na uongozi wa mashujaa ni pamoja na kunipangia nyumba hali itakayonilazimu kuhama ile iliyokuwa chini ya Twanga.
Ninaamini nitafanya vema kazi yangu hii mpya kama ilivyokuwa Twanga ambapo nilidumu kwa muda mrefu na kuchangia kufika hadi hapo nilipoachia, hivyo naomba ushirikiano kwa uongozi, wanamuziki, Wadau na hata ninyi mwaandishi wa habari.Chanzo:fullshangweblog
TAMKO LA VIJANA WA BUKOBA MJINI WAISHIO DAR ES SALAAM
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia Mwenyekiti wa Chama Cha Walemavu wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Simon Andrea, baada ya kufungua Baraza la Vijana wa CCM wilaya hiyo, jana, May 25, kwenye Uwanja wa Mashujaa, wilayani humo. Waliosimama ni baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM walioshiriki ufunguzi huo.
Ujio wa Nape: Kagera Tumedharauliwa na Uzalendo Umedhihakiwa
Tumejaribu kutafakari kwa kina juu ya nini hasa kilimsukuma Nape kufika Kagera na kushiriki mazishi ya muasisi wa TAA, mzalendo na mpigania uhuru aliyetelekezwa na Taifa lake, Dr. Vedasto Kyaruzi na bado ki-ukweli hatujapata majibu.
Tunapata shida kujua dhima ya safari ya Nape kwa kuwa shughuli mahsusi alizozifanya akiwa Kagera zina kinzana kimaadili na kitamaduni na maombolezo ya misiba ya Kiafrika na hasa misiba ya Kihaya. Mjumbe aliyetumwa mahsusi toka mbali kupeleka pole kwenye msiba hategemewi atumie muda wake mwingi majukwaani kufanya siasa, tena katika mazingira ya ugenini lakini kwenye maeneo yale yale msiba unapoendelea. Kwa mpita njia ambaye amefahamishwa tukio na akahiari kufika msibani, akiendelea na shughuli zake haitakuwa ajabu na hakuna mtu mwenye akili timamu atamshangaa hata kidogo.
Nape aliingia Bukoba tarehe 25/05/2012. Na ni uungwana kukiri kuwa alifika Kashai-Matopeni msibani kutoa salamu za pole. Lakini baada ya hapo alielekea Missenyi ambako tunaarifiwa alikuwa na mikutano ya hadhara. Watanzania mtakumbuka vema kuwa katika mikutano hiyo ndiko Nape alitoa kauli ya kutokuwa tayari kukabidhi nchi kwa wahuni! Labda ili Watanzania muweze kupima vema uelewa na akili za Nape, tuwafahamishe kuwa Missenyi ndiko iliko Kyaka na ambako maziko ya Dr. Kyaruzi yamefanyika. Tunashindwa kuelewa, hiyo mikutano ilikuwa safisha njia ya mazishi au inahusiana vipi na mtu aliyepeleka ujumbe wa maombolezo?
Linalochanganya zaidi ni hili la Jumamosi tarehe 26/05/2012. Hii ndiyo siku ambayo Dr. Kyaruzi alipumzishwa rasmi kaburini alale kwa amani. Lakini kwa Nape akiwa Kyaka hii ilikuwa siku maalumu ya kufungua matawi na kutangaza operation yake mpya ya kisiasa iitwayo “Vua Gamba, vua Gwanda, Vaa Uzalendo”. Katika hili, ukiachilia ukinzani wa matukio kimaadili na kitamaduni, tunapata mishangao mingine; hivi Nape alikwenda Kyaka kuzika au kuzindua operation ya kisiasa? Na Je, huyu kijana anahubiri uzalendo upi? Uzalendo usiokuwa na utamaduni, Uzalendo wa kuwatelekeza na kushindwa kuwaenzi watu waliopigania uhuru wa nchi hii? Kama huo ndiyo uzalendo anaohubiri Nape, basi hauhitaji operation wala kampeni maana tayari tunao magwiji. Na hapo kwa tafsiri hii, ujio na matukio ya Nape kwenye maeneo ya msiba huu vinanapata maana halisi.
Katika Taarifa ya Uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Chama Tawala kimearifiwa kuwa moja ya kosa lililofanyika ni kumteua mgombea ambaye mila hazikuwa zinampa fursa na tafsiri njema kufanya shughuli kama ya siasa katika muda mfupi baada ya msiba wa Baba yake. Ikiwa kosa hili la Kitamaduni limechangia Chama kupoteza Jimbo, basi pia chama kiwe tayari kwa makosa ya Nape kupoteza zaidi ya Kijiji cha Burifani na Kata nzima ya Kyaka. Na hatutoshangaa iwapo Nape au Taasisi iliyomtuma ikishindwa kuomba radhi!
Mbali na vioja vya Nape hapo juu, kwa wasifu wa marehemu Dr. Kyaruzi, kila mmoja atakubaliana nasi kuwa Taasisi yoyote (iwe dola au chama) kuwakilishwa na mtu wa ngazi ya Nape ni dharau ya hali ya juu na ichukuliwe ni dhihaka si kwa jamii iliyostaharabika tu, bali hata kwa watu walipendao Taifa lao na kuuenzi Uzalendo. Inakuwa vigumu kuamini kuwa pamoja na ugumu wa ratiba, Rais alikosa muwakilishi makini wa hadhi inayobeba uzito sawia na mchango wa Dr. Kyaruzi katika Taifa hili. Tukio hili linaleta hisia za ubaguzi wa Taasisi za dola na chama katika kutoa uzito kwenye majanga, matatizo na misiba ya watu wa Taifa hili. Ni majuzi tu Taifa lilipotelewa na Mcheza Sinema nguli ambaye hapo awali hakuwahi kupata heshima yoyote ya Kitaifa. Lakini tuliona jinsi viongozi wa Serikali na Chama walivyohamia msibani na Serikali kujipa jukumu la kuubeba msiba na shughuli za mazishi. Haikupita muda, Rais akiwa ziarani Marekani, Rais wa Malawi alifariki duniani. Pamoja na uchovu wa safari tulimwona Rais akiingia nchini na kutoka kuwahi mazishi ya Rais wa nchi jirani. Kulingana uzito na umuhimu uliowekwa na Rais katika msiba huu, hakusubiri hata atatue matatizo makubwa yaliyokuwa yanaikabili serikali yake kiasi cha kutishiwa kuanguka. Lakini pia ni kawaida kusoma taarifa za Rais anazoandika katika mitandao ya kijamii (MyKj) kila anapoelekea kwenye misiba ya watu wa kawaida walioko katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam. Hili linatuongezea huzuni na kutuongoza kuamini kuwa misiba ya watu wa maeneo nje na Dar es Salaam haigusi hisia za Rais hata kama ni ya Watu waliotoa mchango mkubwa kwa Taifa hili. Haya yaliyotokea kwa Dr. Kyaruzi alimanusura yatokee pia kwenye msiba wa MKUU wa Majeshi Mstaafu Jenerali Ernest Mwita Kyaro. Marehemu Mwita alifariki siku chache baada ya mazishi ya Kanumba na msiba wake ulikosa sura ya Kitaifa. Isingekuwa kelele za wana-Mitandao ya Kijamii (MyKj) na wahandishi wa habari, hata Bunge lisingesimama kwa dakika moja kutoa salamu. Tabia hii ya kutelekeza wazalendo wa Taifa hili inaonekana kumea kwa kasi. Na uthaminisho wa serikali kwa watu wa Dar es Salaam unaonekana kuwa juu kuliko wa wale walioko nje ya Dar es Salaam.
Kwa Tamko hili tunamtaka Nape Nnauye, Katibu Mwenezi wa CCM kama kweli alikuja kuwakilisha Taasisi yoyote katika msiba wa Dr. Kyaruzi, basi aiombe radhi jamii yetu kwa dharau kubwa aliyoonyesha katika msiba huu. Na kama alikuwa mpita njia tu, basi atujuze ili Jamii na historia ya Taifa imwandike rasmi Dr. Kyaruzi kama muasisi wa TAA na mzalendo aliyepigania uhuru wa Taifa lake ambaye hakuenziwa wakati wa uhai wake na hata mazishi yake hayakuhudhuriwa na mwakilishi wa Kitaifa.
Na mwisho tunamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, yeye kama Taasisi awe Rais wa Watanzania wote; wa Dar es Salaam na Mikoani.
Asiye na Utamaduni ni Mtumwa. Tanzania ni Moja
Imetolewa na:
Erick Mwemezi Kimasha
Mhamasishaji Jamii Mkuu
Vijana wa Bukoba Mjini Waishio Dar es Salaam
Barua Pepe: ekimasha@ksgroup.co.tz
Simu: 0713-177-372
Tarehe: 27/05/2012
Monday, May 28, 2012
JK opens historic AfDB meeting in Arusha today
President Jakaya Kikwete is today set to officially open a five-day historic annual African Development Bank (AfDB) meeting here, which will be attended by ten Heads of State from African and European countries.
Ngosha Magonya who is the Commissioner of External Finance in the Treasury said the meeting will also bring on board 80 bank’s governors, more than 3,000 bankers and financial experts from across the world.
“This will be an important meeting to our nation and Arusha in particular, as it will explore a number of business opportunities for Tanzania’s small and medium enterprises,” he said.
Magonya said that some entrepreneurs will also benefit from the large number of people who will gather in Arusha as they will get time to go for shopping.
The official said the AfDB annual meetings will be held under theme: “Africa and the Emerging Global Landscape: Challenges and Opportunities”.
Sunday, May 27, 2012
MAKAMU WA RAIS DK. GHARIB BILAL AZINDUA VITABU VIWILI VYA ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA CCM YUSUPH MAKAMBA
Makamu wa Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wageni waalikwa na wanachama wa CCM, waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa vitabu viwili vya Binadamu na Kazi na Ukweli kwa mujibu wa Biblia, na Kurani Tukufu, Suna za Mtume na Sheria za nchi, vilivyotungwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba. Hafla hiyo iliyofanyika leo Mei 27, 2012 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, imefanyika sambamba na hafla ya kumpongeza kwa kuitumikia nafasi yake ya Katibu Mkuu wa CCM hadi anastaafu
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjve6doTaQ1v0OloYry8_NTbtikw0gAgtilLff7E8JER9KnaRPAazwOhMn0NO9SCilbM6GVgs6NgHjPxX2b5r07ar1HEsobYKdpNunQZe6L_c1ikX46UUhBcjYqkWcbMWgmXhaGvV3Q8qQ/s640/04.jpg)
Makamu wa Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akikata utepe kuzindua kitabu cha Ukweli kwa Mujibu wa Biblia, Kuran Tukufu, Suna za Mtume na Sheria za Nchi, kilichotungwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba (kulia) wakati ya uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo Mei 27, 2012, sambamba na hafla ya kumpongeza kwa kuitumikia nafasi yake ya Katibu Mkuu wa CCM hadi anastaafu. Kushoto ni Mke wa katibu huyo, Mama January Makamba.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhHGD8dHDnjR5E2pxXNmATx37rQf0znCnYjkQzL5sktR3DVrD_OVL1SqYvPOqOaAbJZ1-8JWUEDCRcT7Jv4ssTrhcobVv-nm00y_XdRYDN2Dg5m6nlecWOYTMlnW-TgzSmdhlfjdSsjsQM/s640/02.jpg)
Makamu wa Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akikata utepe kuzindua kitabu cha Binadamu na Kazi, kilichotungwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chamamcha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba (kulia) wakati ya uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo Mei 27, 2012, sambamba na hafla ya kumpongeza kwa kuitumikia nafasi yake ya Katibu Mkuu wa CCM hadi anastaafu. Kushoto ni Mke wa katibu huyo, Mama January Makamba.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0DOYj5LCkRxJC8QRI39j4rTBEFqO6QPdpSuYbgixACKT4TUmgx8Fgqx6iFL2vcy2GM9yyJQ36Vsw1xMCCTkDZWO7mR1HlgLYaj_9m2KION7ZngPgjWIHoguqlbf2zfVSuBUIautqhBNg/s640/03.jpg)
Makamu wa Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akionyesha Kitabu cha Binadam na kazi baada ya kukizindua kitabu hicho kilichotungwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba (kulia) wakati ya uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo Mei 27, 2012, sambamba na hafla ya kumpongeza kwa kuitumikia nafasi yake ya Katibu Mkuu wa CCM hadi anastaafu. Kushoto ni Mke wa katibu huyo, Mama January Makamba...
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWj3jKrqfdzqj-qbMzEmq_yNmAydJXLGXci17LG-k378Yn-UENZIqg0OrTKIMejMIA0mn4CxIHPW5A-CqM6OKGbyaknWgqcgraegTNMamDinbeA57fuCo2ZEhBi09hHDJTbn3cix1DvtE/s640/05.jpg)
Makamu wa Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akionyesha Kitabu cha Ukweli kwa Mujibu wa Biblia, Kuran Tukufu, Suna za Mtume na Sheria za Nchi, baada ya kukizindua kitabu hicho kilichotungwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Yusuph Makamba (kulia) wakati ya uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo Mei 27, 2012, sambamba na hafla ya kumpongeza kwa kuitumikia nafasi yake ya Katibu Mkuu wa CCM hadi anastaafu. Kushoto ni Mke wa katibu huyo, Mama January Makamba...
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjlGed30CuebEcLe4TwaOJvNezu6DTWGhBqe2a45GqIuSJulQFFQGfOHBmfVTo1rxW2RK8N6wmOk0zCdiw-Iups5tnnDyY81kamix-VgH0vqu-w4ZzaRhpWBpjOTPp8VR6h4_sVe3YZzZI/s640/06.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yusuph Makamba, wakati wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa vitabu vya Ukweli kwa Mujibu wa Biblia, Kuran Tukufu, Suna za Mtume na Sheria za Nchi na Binadam na kazi, vilivyotungwa na Katibu huyo. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 27, kwenye Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam...
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg6VWSTNojJavsGQY8364Vytse7__piaL6UMQ4ZSZ2w3WqYtlASplLp8rUCB2P7rJcZ8C_v_x3xg_ThBOXxJHK8O28AL-mx38uFdVDrpD1CM53uwveh8N9_iv9kSGQEimxbIt-pU5_NZgk/s640/07.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg10d1Uy3Dj-nLLQvK6V4N4ywS02Ijuc4TaSZUs338-TUHdKQZVTddsW03kWloP-l2gJJASF1RfzJVR4L-j1qwGe2VzmpQip0WDQBcFsvLplpedeU4ZLX5OjPiVSnfNJC9J8MQ7RIhqym8/s640/08.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgulFRxK7Of6igSKiWO_IgUxVhpjfBx23oWn1isn05QRGHtRfWgCtDOusE_7VXBEITrFMwxSmVPMZwdthciOxgBsCzD03-d9Zl4fujHqqxnLFzZUKppytUIzIW8FeA1ADQzwJdxJeskYrA/s640/09.jpg)
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais
ZANZIBAR HALI BADO NI TETE MABOMU YA MACHOZI YAENDELEA KURINDIMA TOKEA JANA JIONI HADI ASUBUHI YA LEO
Hizi ni baadhi ya vurugu zilizotokea jana Mjini Zanzibar huku mabomu ya machozi yakirindima na kuendelea kupigwa na polisi wakati wa vurugu zilizoshababishwa na kundi kubwa la watu kwenda kuvamia kituo cha polisi ili kushinikiza kiongozi wao aliyeshikiliwa na jeshi la polisi aachiwe huru
Picha askari wa kutuliza ghasia akiwa tayari kwa mapambano n awananchi wa zanzibar ambao inasemekana walivamia kituo cha polisi wakiwa na silaha za jadi kama vile rungu na mapanga
Hali tete bado inaendelea asubuhi ya leo mjini zanzibar huku polisi wakiwatawanya wananchi wa zanzibar lakini wananchi hao wanazidi kuongezeka kwa kutaka kiongozi wao kuachiwa huru na polisi ambapo alikamatwa jana na wananchi hao kuvamia kituo cha polisi jana jioni na hatimaye polisi kutumia mabomu ya machozi tokeaa jana jioni hadi asubuhi ya leo
Wananchi wa Zanzibar wakiwa kwenye maandamano wakati wakielekea kituo cha polisi na kabla machozi ya mabomu hayajaanza kulipuliwa na askari.Picha Zote na Abdulaziz El ShuwehdyJANA JIONI KUNDI KUBWA LA WATU WANAOLIUNGANISHA KUNDI LIFAHAMIKALO KWA JINA LA UAMSHO,AMBALO LIMEKUWA LIKIUPIGA VITA MUUNGANO WA TANZANIA NA ZANZIBAR,LILIVAMIA KITUO KIKUU CHA POLISI CHA MADEMA KISIWANI HUMO JIONI YA JANA NA KUSABABISHA VURUGU KUBWA,WAKITAKA KUACHILIWA KWA KIONGOZI WAO ALIEKAMATWA JIONI YA JANA KWA KUONGOZA MHADHARA BILA YA KUWA NA KIBALI CHA SERIKALI.
HALI HIYO IMESABABISHA VURUGU KUBWA KITUONI HAPO HUKU ASKARI POLISI WA KITUO HICHO WAKILAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI ILI KUWATAWANYA WATU HAO AMBAO WENGI WAO WAKO NA SILAHA ZA JADI AMBAZO NI MARUNGU,MAPANGA NA MAWE ILI KUPAMBANA NA ASKARI POLISI KITUONI HAPO VURUGU HIZO ZIMEENDELEA TENA ASUBUHI YA LEO.
Friday, May 25, 2012
Kamanda Kova azuia maandamano, aruhusu mkuta wa Chadema Jangwani-Dar
CHADEMA kuwasha moto Jangwani leo
na Mwandishi wetu
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kitafanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Wilbord Slaa watahutubia.
Aidha, viongozi wengine wakiwemo wabunge wake 15 ni miongoni mwa watakaoshiriki mkutano huo, akiwemo Mbunge wa Ubungo John Mnyika ambaye juzi, alitangazwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwa mbunge halali baada ya kushinda kesi ya kupinga ushindi wake, iliyokuwa ikimkabili.
Joto la mkutano huo limepanda kiasi kwamba, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetangaza kuweka ulinzi mkali.
Taarifa ya CHADEMA jana imesema kuwa, ingawa Mahakama Kuu imewapatia ushindi wabunge wake, Tundu Lissu, John Mnyika, Gervas Mbasa na wengine waliopingwa, leo katika mkutano huo itaeleza umuhimu wa mabadiliko ya kimfumo katika mhimili huo, na katika utendaji kazi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), ambayo chama hicho kinataka iwe chombo huru katika kutekeleza majukumu yake nyeti mbalimbali, ikiwemo kusimamia uchaguzi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, alidai kunahitajika mabadiliko ya kimfumo kwa sababu kumekuwa na athari kubwa katika maendeleo ya wananchi, na pia kikwazo cha kuweka madaraka ya uendeshaji wa nchi mikononi mwa umma kama inavyotamkwa katika ibara ya 8 ya katiba ya sasa.
“Tunataka wananchi wajitokeze kwa wingi kusikiliza masuala mbalimbali, zikiwemo hoja juu ya umuhimu wa kufanya mabadiliko ya kimfumo kupitia uandikwaji wa katiba mpya, waje wajue namna ambavyo ubovu wa katiba ya sasa umechangia kwa kiasi kikubwa matatizo makubwa yanayotukabili kama taifa, ikiwemo umaskini, ujinga, maradhi, ufisadi na CCM yenyewe,” alisema Mnyika.
Alidai kuwa katika mkutano huo, watazindua kampeni ya ‘kuiamsha Dar es Salaam’, ikiwemo kaulimbiu ya ‘Vua Gamba, Vaa Gwanda’ inayotarajiwa kuwapokea viongozi na wanachama wengi kutoka CCM.
Aliongeza kuwa, tofauti na CCM ambayo imeanza mchakato wa katiba kwa kujifungia na kutoa misimamo ya mamlaka za chama bila hata maoni ya wanachama wake nchi nzima, CHADEMA itatumia fursa hiyo kutoa elimu ya uraia kwa umma juu ya sheria ya mabadiliko ya katiba, ili kuwezesha umma kumiliki mchakato na hivyo taifa lipate katiba bora.
Mbali na Mnyika, wabunge wengine watakaoonekana leo ni pamoja na Peter Msigwa, Ezekiah Wenje, Tundu Lissu, Grace Kiwelu, Halima Mdee, Rose Kamili, Mhonga Said, Suzan Kiwanga, Joyce Mkya, Godbless Lema na Meya wa Manispaa ya Musoma, Alex Malima Kasurula.
MVUTANO POLISI, CHADEMA
Hata hivyo, pamoja na Jeshi la Polisi kuruhusu kufanyika kwa mkutano huo, kumezuka mvutano kati ya pande hizo mbili kuhusu suala la wanachama kufanya matembezi ya hiyari kutoka kila kona ya Jiji la Dar es Salaam kuelekea Jangwani.
Wakati CHADEMA wakitangaza ramani yatakapopita matembezi hayo, polisi imeyapiga marufuku kwa madai kwamba hakuna sheria yoyote inayoruhusu chama cha siasa kufanya matembezi au maandamano.
Awali, CHADEMA ilituma maombi ya maandishi kwa Jeshi la Polisi kuruhusu matembezi hayo ya amani, kutoka sehemu mbalimbali za jiji hadi viwanja vya Jangwani panapofanyika mkutano wa hadhara leo.
Lakini jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema, wanaruhusu kufanyika kwa mkutano huo, na wamejiandaa kikamilifu katika ulinzi, lakini si kwa matembezi.
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, CHADEMA iliwasilisha barua ya kuomba kibali cha kufanya mkutano, lakini kabla ya kujibiwa, kilipeleka barua nyingine yenye lengo la kupewa kibali cha matembezi ya amani.
Kova alidai kuwa, mwanachama yeyote atakayekaidi amri hiyo, atachukuliwa hatua za kisheria, na kuonya kuwa watu wasidanganyike kufanya matembezi hayo, ila kila mtu anayo haki ya kwenda katika mkutano kwa namna ya kawaida.
Hata hivyo, CHADEMA imepinga na kudai kuwa hayo si maandamano, bali matembezi maalum kutoka kwenye maeneo ya jiji kwenda viwanja vya Jangwani, ikizingatiwa kuwa hali ni ngumu na si kila mtu mwenye uwezo wa kumudu gharama za usafiri.
Chama hicho kimedai kuwa, Watanzania wanayo haki kikatiba kufanya maandamano na mikusanyiko ili mradi hawavunji sheria, na kimetangaza barabara zitakazotumiwa na watu wa majimbo ya Ilala, Ukonga na Segerea, kuwa ni Buguruni, Uhuru, Msimbazi, Morogoro hadi Jangwani.
Watakaotoka majimbo ya Kinondoni, Kawe na Ubungo, watakutanika katika bustani ya Magomeni, kupitia barabara ya Morogoro hadi Jangwani, wakati wale wa Kigamboni, wataanzia Kivukoni, kupitia Posta ya zamani, Makao Makuu ya Jiji, barabara ya Morogoro hadi Jangwani.
Wale wa Temeke, wataanzia Mwembeyanga, kupitia barabara ya Mandela, Buguruni na kukutana na wale wa majimbo ya Ilala na kuelekea Jangwani.
BREAKING NEWS: SIMBA KUMUUZA OKWI AUSTRIA MILIONI 750
![]() |
Okwi |
MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Emmanuel Arnold Okwi anaweza akauzwa kwa klabu moja ya Austria kwa dau la dola za Kimarekani 500,000 (zaidi ya Sh. Milioni 750 za Tanzania) na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyewahi kuuzwa kwa ‘bei chafu’ zaidi Simba SC.
Kwa sasa, Mbwana Ally Samatta aliyeuzwa kwa dau la dola za Kimarekani 100,000 kwenda Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) msimu uliopita, ndiye anashikilia rekodi ya mchezaji wa Simba kuuzwa bei ghali zaidi.
Habari za ndani kutoka Simba, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata jioni hii zinasema kwamba, Okwi mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, mwenye umri wa miaka 19 aliyetua Simba mwaka 2010 akitokea SC Villa ya Uganda anatakiwa na klabu hiyo kwa dau hilo tamu.
Ofa hiyo tayari iko mezani kwa Simba na kwa sasa inafanyiwa kazi kabla ya wakati wowote kutangazwa rasmi kuuzwa kwa mchezaji huyo, aliyesajiliwa na Wekundu wa Msimbazi, kwa dau la dola za Kimarekani 5000.
JK: More funds will go into projects for poor
President Jakaya Kikwete yesterday promised that programmes and policies that are broad based and pro poor will be implemented so as to ensure that every Tanzanian enjoys the benefits of economic growth.
President Jakaya Kikwete
The President made the remarks yesterday in Dar es Salaam when opening a one-day conference on unleashing growth potentials in Tanzania to create an inclusive growth, organised by the Economic and Social Research Foundation (ESRF).
In his speech read by the Deputy Minister for Finance Saada Salum, he said the government will increase resources and strengthen institutions such as local government authorities that have direct dealings with the ordinary people.
President Kikwete who is in Dodoma for other government activities said that is the only way to make majority people enjoy the benefits of economic growth.
“We will continue investing more in social services and improve the quality of education, health and social safety nets for vulnerable persons and communities,” he said
He noted that despite impressive growth and macroeconomic stability, the majority of people remained poor. Statistics show that from 2001 to 2007 the overall household poverty fell by a marginal rate of 2 percent from 35.7 percent to 33.6 percent in Mainland Tanzania and from 49 percent to 44.7 percent in Zanzibar.
TFF NA HALI YA MAMBO NDANI KLABU YA YANGA
Aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Bw. Loyd Nchunga.
Kwa vile wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji ya Yanga akiwemo Mwenyekiti wa kamati hiyo Lloyd Nchunga wamejiuzulu, Kamati ya Uchaguzi ya Yanga imeliandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikitaka mwongozo juu ya hilo.
Kwa kuzingatia hilo, TFF imepeleka suala hilo kwa kamati yake ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ili itoe maoni yake kisheria ya nini kinafanyike kuhakikisha Yanga inaendelea na shughuli zake kama kawaida.
MAKAMU WA RAIS DKT BILAL KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MJINI BOTSWANA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib
Bilal na Mama Asha Bilal, wakiingi kwenye ukumbi wa tafrija ya chakula
cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Botswana Lt General Seretse Khama
kwa viongozi wakuu wa Nchi za Afrika waliohudhuria mkutano wa siku
mbili kuhusu maendeleo endelevu ya Bara la Afrika Nchini Gaborone
Botswana.
Bilal na Mama Asha Bilal, wakiingi kwenye ukumbi wa tafrija ya chakula
cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Botswana Lt General Seretse Khama
kwa viongozi wakuu wa Nchi za Afrika waliohudhuria mkutano wa siku
mbili kuhusu maendeleo endelevu ya Bara la Afrika Nchini Gaborone
Botswana.
(PICHA NA VPO)
Makamu wa Raisa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib
Bilal kushoto, Rais wa Liberia Mhe. Ellen Jonson na Rais wa Botswana
Mhe. Lt General Seretse Khama wakiwa kwenye tafrija ya chakula cha
jioni kilichoandaliwa na Rais wa Botswana kwa Viongozi wakuu wa Afrika
waliohudhuria mkutano wa siku mbili kuhusu maendeleo endelevu ya Bara
la Afrika jana jioni.
Bilal kushoto, Rais wa Liberia Mhe. Ellen Jonson na Rais wa Botswana
Mhe. Lt General Seretse Khama wakiwa kwenye tafrija ya chakula cha
jioni kilichoandaliwa na Rais wa Botswana kwa Viongozi wakuu wa Afrika
waliohudhuria mkutano wa siku mbili kuhusu maendeleo endelevu ya Bara
la Afrika jana jioni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib
Bilal na mkewe Mama Asha Bilal wakiwa kwenye tafrija iliyoandaliwa na
Rais wa Botswana Lt. General Seretse Khama kwa ajili ya viongozi wakuu
wa Nchi za Afrika waliohudhuria mkutano kuhusu maendeleo endelevu kwa
Bara la Afrika
Bilal na mkewe Mama Asha Bilal wakiwa kwenye tafrija iliyoandaliwa na
Rais wa Botswana Lt. General Seretse Khama kwa ajili ya viongozi wakuu
wa Nchi za Afrika waliohudhuria mkutano kuhusu maendeleo endelevu kwa
Bara la Afrika
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akizungumza na baadhi ya
wajumbe waliohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu
maendeleo endelevu kwa bara la Afrika unaoendelea mjini Gaborone
Botswana
wajumbe waliohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu
maendeleo endelevu kwa bara la Afrika unaoendelea mjini Gaborone
Botswana
Wasanii wa kikundi cha ngoma za utamaduni nchini Botswana wakitumbuiza
kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu maendeleo endelevu ya
Bara la Afrika unaoendelea leo mjini Gaborone Botswana.
kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu maendeleo endelevu ya
Bara la Afrika unaoendelea leo mjini Gaborone Botswana.
Wednesday, May 23, 2012
WANANCHI WENYE HASIRA WAUWA MAJAMBAZI WATATU JIJINI ARUSHA
NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA
WANANCHI wenye hasira katika eneo la Ngusero Ndani ya manispaa ya Arusha wamewaua majambazi matatu kwa silaha za jadi mara baada ya majambazi hayo kubainika kuwa wanapanga mbinu mbalimbali za kuvunja nyumba
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Bw Thobias Andengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea alfajiri ya saa kumi za asubui ambapo majambazi hayo yalifika katika eneo hilo huku yakiwa ndani ya gari
Kamanda Andengenye alisema kuwa mara baaada ya majambazi hayo kufika katika eneo hilo la tukio wakiwa na gari aina ya Corola lenye namba T830 AHU walianza kuzunguka zunguka katika eneo hilo ili kupanga nyumba ambayo wanaingia hali ambayo iliwashitua wananchi
Alifafanua kuwa mara baada ya wananchi kutilia shaka gari hilo ambalo lilikuwa na majambazi hao waliamua kuwaweka chini ya ulinzi na kukagua gari hilo ambapo walikutana na Silaha za jadi pamoja na silaha nyingine ambazo ni za kuvunjia nyumba hali ambayo ilisababisha waweze kupigwa sana na wananchi hao
“inavyosemekana ni kwamba hawa majambazi walikuwa wameshazunguka san a na gari lao kwa muda mrefu sana na sasa mara baada ya kuhisiwa wananachi waliamua kujichukulia sheria mkononi na kisha kuanza kuwapiga sana hali ambayo ilisababisha Mauti yao hapo hapo”alisema kamanda Andengenye.
Aliongeza kuwa mara baada ya Jeshi la Polisi kufika katika eneo hilo waliweza kugundua kuwa kati ya majambazi hayo matatu mawili yalikuwa yanatafutwa na jeshi hilo bila mafanikio kwa kuwa walikuwa wanatuhumiwa kwa makosa ya unyanganyi wa kutumia silaha ndani ya maeneo mbalimbali ya Mji wa Arusha
RAIS JAKAYA KIKWETE APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO WA BALOZI WA RWANDA NCHINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amezitaka Tanzania na Rwanda kuongeza kasi katika mipango ya kuanzisha miradi ya pamoja ya miundombinu, ukiwamo ujenzi wa reli mpya kuunganisha nchi hizo mbili.
Rais Kikwete ametoa wito huo wakati alipozungumza na Balozi mpya wa Rwanda katika Tanzania, Mheshimiwa Benjamin Ruganguzi, baada ya balozi huyo kuwasilisha kwa Rais Kikwete hati zake za utambulisho katika halfa fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es salaam, leo, Jumanne, Mei 22, 2012.
Baada ya kuwa amemkaribisha Tanzania kwa kumhakikishia kuwa uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda ni mzuri na unaendelea kuwa wa karibu zaidi, Rais Kikwete amemwambia Balozi Ruganguzi, “Kazi kubwa na ya kwanza Mheshimiwa Balozi iwe ni kusaidia kuhakikisha kuwa mradi wa ujenzi wa reli unaanza mapema iwezekanavyo.”
Tanzania na Rwanda zimekubaliana kujenga reli kati ya Isaka, Tanzania hadi Kigali, Rwanda, reli ambayo itaunganisha pia nchi jirani ya Burundi. Nchi hizo mbili zinafanya jitihada za pamoja kuwasiliana na kuzungumza na wafadhili na makampuni binafsi ya kimataifa kuangalia uwezekano wa kupatikana kwa uwezeshwaji wa kujengwa kwa reli hiyo.
Katika mazungumzo yao, Rais Kikwete na Balozi Ruganguzi pia wamekubaliana kuanza ujenzi ama kukarabati miundombinu nyingine inayotakiwa kuanzishwa ama inayotumiwa kwa pamoja na nchi hizo ukiwamo ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwenye Mto Rusumo, kupanua daraja linalounganisha nchi hizo kwenye mto huo na pia kukarabati Reli ya Kati inayosafirisha mizigo ya Rwanda.
Ili kuhakikisha kuwa anakuwa na ufutiliaji wa karibu juu ya miradi hiyo, Rais Kikwete amemshauri Balozi Ruganguzi kuhakikisha kuwa anatembelea bila kuchoka Wizara ya Uchukuzi pamoja na taasisi zake kama vile Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Bandari ya Dar es Salaam.
“Ushauri wangu kwako ni kwamba jipe muda wa kuwatembelea mara kwa mara maofisa wa Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake kama vile TRC na Bandari ili uweze kupata habari za uhakika kuhusu miradi yetu ya pamoja,” Rais amemwambia Balozi Ruganguzi.
Rais pia amemhakikishia balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuhudumia mizigo ya Rwanda kupitia Bandari ya Dar es Salaam na kutumia Reli ya Kati na barabara za Tanzania.
Hakuna atakayepora ardhi ya wananchi – Rais Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mipango mikubwa ya kuendeleza kilimo inayopangwa ama tayari inaendeshwa na Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi hailengi kupora adhi ya wananchi na badala yake inalenga kuongeza thamani kwenye ardhi hiyo kwa manufaa ya pande zote zinazojihusisha na kilimo.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa siyo wawezekezaji wote wanaotaka kuingia katika sekta ya kilimo wataokuwa wanaendesha shughuli ya moja kwa moja ya kilimo bali watawekeza katika huduma na raslimili za kuhudumia na kuunga mkono maendeleo ya kilimo.
Rais Kikwete ameyasema hayo, Jumanne, Mei 22, 2012, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Biashara wa Marekani, Mheshimiwa Michael Camunez ambaye yuko katika ziara ya Tanzania tokea Jumamosi iliyopita.
Rais Kikwete amesema kuwa pamoja na kwamba Serikali inafanya jitihada kubwa za kuendeleza kilimo, pengine kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Tanzania huru, bado ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kuwa inaendelea kulinda ardhi ya wakulima wadogo na kuwawezesha kunufaika na uwekezaji wa sekta binafsi ndani ya ardhi yao wenyewe.
Rais Kikwete amesema pia kuwa ni vigumu kwa wawekezaji wa sekta binafsi kupora ardhi ya wananchi katika Tanzania kwa sababu kila wilaya katika Tanzania ina benki ya ardhi ambayo ndiyo itatolewa kwa wawekezaji wa sekta binafsi na wala siyo ardhi ya wananchi.
“Sekta binafsi inakuja kuwekezaji katika kilimo na wala siyo kupora ardhi ya wananchi. Wale wawekezaji wa sekta binafsi watapewa ardhi kutoka kwenye benki za ardhi za wilaya mbali mbali na hakuna atakayegusa ardhi ya wananchi,” amesema Rais Kikwete katika mazungumzo na Naibu Waziri huyo ambaye nchi yake ya Marekani ni moja ya nchi ambayo makampuni yake yanataka kuingia katika maendeleo ya kilimo katika Tanzania.
Kuhusu sekta binafsi kuwekeza katika kilimo, Rais Kikwete amesema kuwa siyo kila mwekezaji atakuja kulima. “Wengine watakuja kuwekeza katika kuzalisha mbegu bora zaidi, wengine kama kampuni ya Yara watakuja kuwekeza katika uzalishaji na usambazaji wa mbolea, wengine watakuja kuingia katika uzalishaji na usambazaji wa mashine za kilimo, wengine katika uzalishaji wa madawa ya kilimo na wengine katika kutoa huduma za kifedha kwa wakulima,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Wengine wanaweza hata kuwekeza katika viwanda vya kuongeza thamani kwenye mazao ya wakulima na ya kilimo.”
Tuesday, May 22, 2012
Rais Dkt.Jakaya Kikwete amuapisha Waziri wa nchi Ofisi ya Rais asiyekuwa na wizara maalumu Profesa Mark Mwandosya Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi
Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum Profesa Mark Mwandosya akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.Na watatu kulia ni Karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu.
Profesa Mwandosya akipokea miongozo ya kazi baada ya kula kiapo ikulu leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza na kumtakia mafanikio Profesa Mwandosya muda mfupi baada ya kumuapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsaidia Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais asiye na Wizara maalumu Profesa Mark Mwandosya kushuka katika ngazi za ikulu baada ya kumuapisha leo asubuhi.
Waziri Profesa Mark Mwandosya akiwa katika mazungumzo na Rais Dkt.Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya kula kiapo ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha na Freddy Maro)
Monday, May 21, 2012
RAIS AKUTANA NA UONGOZI WIZARA YA KILIMO MALIASILI, NA MIFUGO UVUVI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo na
Maliasili,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko
Ikulu Mjini Zanzibar jana,(kushoto) Makamo wa kwanza wa Rais Maalim
Seif Sharif Hamad. [ Picha na Ramadhan Othman,IKULU.]
Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo na
Maliasili,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko
Ikulu Mjini Zanzibar jana,(kushoto) Makamo wa kwanza wa Rais Maalim
Seif Sharif Hamad. [ Picha na Ramadhan Othman,IKULU.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko Ikulu
Mjini Zanzibar jana, [ Picha na Ramadhan Othman,IKULU.]
Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi,katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Wizara hiyo huko Ikulu
Mjini Zanzibar jana, [ Picha na Ramadhan Othman,IKULU.]
Subscribe to:
Posts (Atom)