Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi Mdogo wa Norway nchini Tanzania, Svein Baera, baada ya kuwasili kwenye ofisi za ubalozi huo zilizopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutia saini Kitabu cha Maombolezo, kufuatia tukio la kuripuliwa kwa bomu kulikofanyika nchini Norway wiki hii na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 70. Katikati ni Balozi Mdogo wa ubalozi huo anayehusika na masuala ya Utawala, Tom Elversather. |
No comments:
Post a Comment