Waziri Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo,Omar Yussuf Mzee
---
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Hatimaye Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo baada ya mjadala mkali katika Baraza hilo.
Bajeti hiyo imepitishwa baada ya Serikali kukubali hoja ya Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Hamza Hassan Juma kutaka kuundwe Kamati teule kwa ajili ya uchunguzi wa eneo ambao ilikuwa ijengwa Makao Makuu ya Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB) ambalo halikutumika na kupewa mtu mwengine binafsi.
Wawakilishi wengi waliochangia waliikosoa Wizara hiyo katika maeneo kadhaa ikiwemo suala la Tume ya Pamoja ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi, Idara ya Uhakiki mali.
Katika michango yao, Wawakilishi walisema kwamba suala la Tume ya Pamoja ya Fedha linahitaji kutolewa maelezo ya kina kujuwa mgawanyo wa mapato na matumizi kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, walisema umefika wakati TRA kuiachia ZRB kodi kukusanya kodi kwa upande wa Zanzibar na pia kutowanyanyasa wafanyabiashara hasa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Wakati Baraza lilipokaa kama Kamati nzima, Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Hamza Hassan Juma aliiomba Serikali kuunda Kamati kufuatilia tatizo la ardhi iliyokuwa imetolewa kwa Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB) kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Makao Makuu yake ambayo hata hivyo, ZRB waliikataa.
Waziri Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo,Omar Yussuf Mzee akitoa ufafanuzi wa hoja ya Mwakilishi Hamza, alisema haoni sababu ya kuunda kwa Kamati ya uchunguzi.
Majibu hayo hayakumridhisha Mwakilishi Hamza na kuiomba Kamati nzima ya Baraza la Wawakilishi kurejea katika Baraza kuamua hoja yake jambo ambalo lilisababisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Mwinyihaji Makame Mwadini kuahidi suala hilo litafanyiwa kazi.
Hata hivyo, Mwakilishi Hamza alikataa na kusisitiza haja ya kuundwa kwa Kamati Teule ambapo katika hatua hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed aliposimama na kukubali hoja ya kuunda Kamati teule.Baraza limeidhinisha jumla ya matumizi ya shilingi bilioni 174.86 ambazo shilingi 47.02 bilioni ni kwa matumizi ya kawaida kwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi
No comments:
Post a Comment