Thursday, September 29, 2011

ZFA CHAILILIA SERIKALI KUHUSU UDHAMINI WA LIGI KUU



Na Hamad Hija-Maelezo Zanzibar
KATIBUmsaidizi wa chama cha soka cha Zanzibar ZFA Masuod Attai ameiomba Serikali ya Mapinduzi kuzungumza na taasisi na kampuni mbali mbali nchini ili ziweze kudhamini ligi kuu ya Zanzibar.
Masuod Attai alitoa ombi hilo mbele ya Kamati ya Mifugo, Uwezashaji, Habari na utalii ambapo kamati hiyo ilikuwa ikizungumza na viongozi wa vyama vya michezo vya Zanzibar
Amesema kuwa kuna haja kubwa kwa Serikali kuzungumza na makampuni hayo ili kuweza kusaidia kudhamini ligi kuu ya Zanzibar ambayo kwa sasa haina mdhamini.
Akitaja makampuni ambayo Serikali inaweza kuzungumza nayo nakuweza kusaidia, ni pamoja na Kampuni ya Simu ya Vodacom, Zantel, Tigo na Air tel ambapo kampuni hizi zinauwezo wa kusaidia katika masuala mengi yakiwemo ya michezo
Amesema msimu wa mwaka 2008-9 Zantel ilikuwa mdhamini mkuu wa ligi hiyo ambapo kwa sasa wamewaacha mkono hivyo Serikali ni vyema izungumze na makampuni ambayo yapo Nchini ili kuiokoa ligi hiyo.
Amefahamisha kuwa licha ya kuwa na udhamini wa million 120 msimu wa 2008-9 ambazo zilikuwa hazikidhi haja lakini uliweza kusukuma mbele ligi hiyo jambo ambalo kwa sasa limekosekana kabisa
Attai amesema kuendesha ligi kwa msimu mmoja kunagharimu pesa nyingi katika kuendesha na kwa sasa chama cha soka cha Zanzibar hakina pesa hizo kwa ajili ya kugharamia ligi hiyo.
Mbali na kuiomba serikali kufanya hivyo pia Katibu huyo msaidizi wa chama cha soka cha zanzibar ameiomba Serikali kuzisaidia timu ambazo zinawakilisha Nchi katika michezo ya kimataifa.
Amesema kucheza mechi moja kwa timu inalazimu kutumia jula ya shilingi 30milion hivyo Serikali inawajibu mkubwa kuvisaidia vilabu vyetu ili viweze kushiriki kikamilifu katika mashindano yanayovikabili vilabu hivyo.

No comments:

Post a Comment