NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
WIZARA YA Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imejipanga kwa makini ili kuhakikisha kuwa maeneo yote ya wazi yanarudishwa kwa wananchi ambapo matumizi yake yatakuwa kwa manufaa ya watanzania wote.
Aidha wizara hiyo imesema kuwa itatoa muda maalum kwa watu wote walivamia maeneo hayo kuondoka wenyewe na utakapokwisha muda uliopangwa itakuja kubomoa hivyo hakutakuwa na msamaha.(hakuna cha msalie mtume).
Kauli hiyo ilitolewa (leo)jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Maliasili na Mazingira, Abdulkarim Shah, wakati akifunga maonesho ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ya wizara hiyo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa, Mnazimmoja, jijini Dares Salaam.
Shah alitoa kauli hiyo ikiwa ni matazamio ya miaka 50 ijayo ya wizara hiyo huku akisema maeneo hayo yamepangwa kwa faida ya wananchi wote.
“Napenda kusisitiza kwamba taaluma ya upangaji miji inahitajika kutiliwa maanani na serikali haitakubali mipango hiyo kubadilishwa matumizi kiholela. Natoa rai hii kwa jamii kushirikiana na serikali kulinda maeneo ya wazi yaliyoko katika maeneo yao,” alisema Shah.
Aliwataka watendaji husika hasa wa halimashauri kutobalidilisha matumizi ya ardhi .
Aliongeza kuwa wizara hiyo imeandaa mikakati ya kuwa na mipango shahidi ya uendelezaji miji itakayokidhi mahitaji ya idadi kubwa zaidi ya watu watakaoishi mijini.
Pia kuwa na mipango itakayowezesha ujenzi wa miji nadhifu, ya kisasa na endelevu,kuzijengea uwezo halimashauri kusimamia na kudhibiti uendelezaji wa miji na kuwa na mipango ya matumizi ya ardhi kwa kila eneo la makazi nchini.
“ Wizara imedhamiria kuongeza kasi ya upimaji wa ardhi nchini kwa matumizi mbalimbali pamoja na kupunguza gharama za upimaji, ambapo nchi itakuwa imejenga kituo cha kupokea na kusambaza picha za saltillite, vituo vingi zaidi cha upimaji vitajengwa,” alisema.
Makamu Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa wizara hiyo itaanza kutunza kumbukumbu za upimaji na ramani kwa kutumia teknolojia ya kisasa, ambapo sasa inatumika mikoa 15 baadae itakuwa mikoa yote hadi wilayani kulingana na uwezo wa bajeti.
Alisema ili kuwawezesha wananchi kutumia ardhi kama mtaji wizara itahakikisha kuwa mashamba ya wananchi vijijini kote nchini yanabainishwa yanapimwa na wamiliki wake wanapewa hatimiliki za kimila.
Alisema kwa upande wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) limejipanga kujenga nyumba 150,000 katika kipindi cha miaka 50 ijayo na kujenga nyumba kwa ubia kwa kuwashirikisha wawekezaji wengine.
No comments:
Post a Comment