Pichani ni Saed Kubenea, Mkurugenzi na Mwandishi Mwanadamizi wa gazeti la Mwanahalisi.
Taarifa ya awali;
Hivi juzi, Mbunge wa Sumve (CCM,) Mheshimiwa Richard Ndasa alitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu habari iliyochapishwa na gazeti la Mwanahalisi toleo la wiki iliyopita ambazo zilielezea hatua ya bunge kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais.
Ni kufuatia sakata la kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo na kurudishwa tena kazini. Akizungumzia habari iliyochapishwa na gazeti hilo, Mheshiniwa Ndasa alisema kuwa gazeti la Mwanahalisi limechapisha habari za kizushi na za uongo zenye lengo la kufitinisha Bunge na Rais. Aliongeza kusema kuwa wakati Jairo anarudishwa kazini na Katibu Mkuu, Luhanjo, Bungeni mjini Dododma hapakuwa na hatua yoyote ya wabunge kupanga kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais kufuatia kuruhusiwa kwa Jairo kuendelea na kazi.
Akifafanua kuhusu uamuzi wao wa kutolea ufafanuzi na kukanusa habari hiyo, Ndasa alisema wao kama wabunge wa CCM, hawatopenda kuona kiongozi wa nchi anazushiwa habari zisizo na ukweli wowote.
Hapa chini ni maoni ya mwanahabari na mchambuzi wa siku nyingi Nkwazi Mhango;
"Ni umbea na upuuzi kufikiri kuwa wabunge wa CCM wanaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na mwenyekiti wao na serikal yao. Mambo mangapi mazito yamepita na wabunge hao hao hawajapiga kura ya kutokuwa na imani na rais?
Hivi kuna jambo zito kama nchi kukaa kizani kwa miongo nenda rudi huku ikiendeshwa kwa autopilot? Mwanahalisi wameanza kuwa wazushi wa kawaida wanaotumwa na baadhi ya mafisadi baada ya kuwekwa kinyumba na mafisadi hao.
Bila kumung'unya maneno ni kwamba, japo kuna haja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Kikwete na baraza lake la mawaziri, kazi hiyo haiwezi kufanywa na wabunge toka CCM. Hilo haliwezekani na anayedhani linawezekana ajiulize zile mbio na tambo za mafisadi waliojiita wapiganaji dhidi ya ufisadi waliishia wapi zaidi ya kuwa vita baina ya mafisadi."
Nkwazi Mhango
Nkwazi Mhango
No comments:
Post a Comment