Sunday, July 31, 2011

TAIFA STARS KUPAMBANA NA CHAD KOMBE LA DUNIA 2014

Upangaji makundi ya mechi za mchujo kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil ulifanywa jana (Julai 30 mwaka huu) karibu na ufukwe wa Copacabana jijini Rio de Janeiro nchini Brazil ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Jerome Valcke.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Bw. Boniface Wambura imesema, Timu ya Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kundi C Kanda ya Afrika ambalo lina timu za Cote d’Ivoire, Morocco na Gambia. Lakini kabla ya kuingia katika kundi hilo Stars italazimika kucheza raundi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Chad.
Stars ikifanikiwa kuitoa Chad baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini zitakazochezwa kati ya Novemba 11-15 mwaka huu ndiyo itaingia katika kundi hilo la C. Pia mshindi wa kundi C ndiye atakayeingia katika raundi inayofuata kabla ya kupata tiketi ya kwenda Brazil.
Stars ni miongoni mwa timu 29 ambazo kwenye viwango vya ubora vya FIFA vya Julai mwaka huu katika Afrika ziko chini ya timu 24 bora, hivyo kulazimika kuanzia hatua hiyo ya kuchujana zenyewe kabla ya kuingia hatua ya makundi ambayo itachezwa kuanzia Juni 1, 2012 hadi Septemba 10, 2013.
Kwa mujibu wa viwango vya FIFA vya Julai mwaka huu, Tanzania iko katika nafasi ya 127 wakati Chad ni namba 158. Kwa upande wa Afrika, Tanzania ni namba 33 na Chad 43. Nchi 52 kati ya 53 za Afrika zimeingia katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia. Ni Mauritania pekee ambayo haikuthibitisha ushiriki wake.
Timu 10 za juu kwa ubora barani Afrika ambazo zimeongoza makundi 10 ya Afrika katika upangaji ratiba ni Afrika Kusini, Tunisia, Cote d’Ivoire, Ghana, Burkina Faso, Nigeria, Misri, Algeria, Cameroon na Senegal.
Afrika ina nafasi tano kwenye fainali za Kombe la Dunia, huku Ulaya ikiongoza kwa kuwa nazo 13.

Saturday, July 30, 2011

Hatimaye Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Wamepitisha Bajet


Waziri Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo,Omar Yussuf Mzee
---

Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Hatimaye Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo baada ya mjadala mkali katika Baraza hilo.

Bajeti hiyo imepitishwa baada ya Serikali kukubali hoja ya Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Hamza Hassan Juma kutaka kuundwe Kamati teule kwa ajili ya uchunguzi wa eneo ambao ilikuwa ijengwa Makao Makuu ya Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB) ambalo halikutumika na kupewa mtu mwengine binafsi.

Wawakilishi wengi waliochangia waliikosoa Wizara hiyo katika maeneo kadhaa ikiwemo suala la Tume ya Pamoja ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi, Idara ya Uhakiki mali.

Katika michango yao, Wawakilishi walisema kwamba suala la Tume ya Pamoja ya Fedha linahitaji kutolewa maelezo ya kina kujuwa mgawanyo wa mapato na matumizi kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, walisema umefika wakati TRA kuiachia ZRB kodi kukusanya kodi kwa upande wa Zanzibar na pia kutowanyanyasa wafanyabiashara hasa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Wakati Baraza lilipokaa kama Kamati nzima, Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Hamza Hassan Juma aliiomba Serikali kuunda Kamati kufuatilia tatizo la ardhi iliyokuwa imetolewa kwa Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB) kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Makao Makuu yake ambayo hata hivyo, ZRB waliikataa.

Waziri Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo,Omar Yussuf Mzee akitoa ufafanuzi wa hoja ya Mwakilishi Hamza, alisema haoni sababu ya kuunda kwa Kamati ya uchunguzi.

Majibu hayo hayakumridhisha Mwakilishi Hamza na kuiomba Kamati nzima ya Baraza la Wawakilishi kurejea katika Baraza kuamua hoja yake jambo ambalo lilisababisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Mwinyihaji Makame Mwadini kuahidi suala hilo litafanyiwa kazi.

Hata hivyo, Mwakilishi Hamza alikataa na kusisitiza haja ya kuundwa kwa Kamati Teule ambapo katika hatua hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed aliposimama na kukubali hoja ya kuunda Kamati teule.Baraza limeidhinisha jumla ya matumizi ya shilingi bilioni 174.86 ambazo shilingi 47.02 bilioni ni kwa matumizi ya kawaida kwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi

Thursday, July 28, 2011

Kamanda wa waasi auawa Libya


Abdel Fattah Younes alimuasi Gaddafi na kujiunga na waasi
Kiongozi wa kijeshi wa waasi nchini Libya wanaokabiliana wakitaka kumpindua Kanali Muammar Gaddafi ameuawa, baraza la mpito la Libya limesema.
Kiongozi wa baraza hilo Mustafa Abdul-Jalil amesema Jenerali Abdel Fattah Younes ameuawa na watu wanaomuunga mkono Gaddafi, na kiongozi wa watu hao tayari amekamatwa.
Amesema Jenerali Younes aliitwa kwenye mkutano ambapo alitakiwa aeleze kuhusu harakati za kijeshi, lakini aliuawa kabla ya kufika kwenye kikao hicho.
Taarifa zinasema kuwa Jenerali Younes alishukiwa kuwa na uhusiano na majeshi yanayomuunga mkono Gaddafi.
Jenerali Younes ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani ambaye alikimbia na kujiunga na upande wa upinzani mwezi Februari.
Wasaidizi wawili wa Jenerali Younes, Kanali Muhammad Khamis na Nasir al-Madhkur, pia waliuawa kwenye shambulio hilo, Bwana Jalil alisema.
Taarifa ambazo hazikuweza kuthibitishwa zilisema kuwa Jenerali Younes na wasaidizi wake wawili walikamatwa mapema siku ya Alhamisi katika eneo la kaskazini mwa Libya.
Mapema siku ya Alhamisi, waasi walisema kuwa wameteka mji muhimu wa Ghazaya karibu na mpaka wa Tunisia, baada ya makabiliano makali na vikosi vya Kanali Gaddafi.Chanzo ni bbckiswahili

Makamu Wa Rais Aomboleza Vifo Vya Watu 70 Norway


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi Mdogo wa Norway nchini Tanzania, Svein Baera, baada ya kuwasili kwenye ofisi za ubalozi huo zilizopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutia saini Kitabu cha Maombolezo, kufuatia tukio la kuripuliwa kwa bomu kulikofanyika nchini Norway wiki hii na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 70. Katikati ni Balozi Mdogo wa ubalozi huo anayehusika na masuala ya Utawala, Tom Elversather.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo katika ofisi za Ubalozi wa Norway nchini, kufuatia vifo vya watu zaidi ya 70 waliofariki kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea wiki hii nchini humo. Katikati ni Balozi Mdogo wa Norway nchini, Svein Baera (kulia) ni Balozi Mdogo anayehusika na masuala ya Utawala, Tom Elvesather. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Tuesday, July 26, 2011

Rais Jakaya Kikwete Atembelea Kituo Cha Utafiti Naliendele

Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti Dr Geofrey Mkamilo wa kituo cha Naliendele kuhusu zao la muhogo
Rais Jakaya Kikwete akiangalia chupa ya juice iliyotengenezwa na mabibo ya korosho(cashew apple)katika kituo cha Utafiti Naliendele huku Dr Peter Masawe, Mtafiti Kiongozi wa korosho nchini akimpatia maelezo ya ubora wa kinywaji hicho tarehe.

Ni mambo ya Mzee Ernest Paulo Waya




Mzee Ernest Paulo Waya  aliyepigana vita kuu ya pili vya Dunia akiongea na Mbeya Yetu, amesema serikali imewatelekeza na kutowajali kwa chochote na kuwazulumu mafao yao mashujaa hao wa zamani ila huwaona wamaana sana siku ya mashujaa na kuwaita ili washiriki pamoja siku hiyo zoezi hilo likiisha huwatelekeza mpaka mwaka mwingine tena mzee Waya amesema ndiyo maana mwaka huu wenzake wengi hawajaja wapo kujitafutia riziki maana kula yao niyashida sana!

Sunday, July 24, 2011

Zeco:Wazungumzia Kuhusu Matumizi Ya Majenereta Ya Dharura

MENEJA Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Mbarouk akizungumza na Waandishi wa habari vyombo mbalimbali, Ofisini kwake kuhusiana matumizi ya majenereta ya dharura.
WAANDISHI wa habari wakimsikiliza Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme alipokuwa akitowa maelezo ya mwenendo wa matumizi ya Umeme kwa Wateja wa bidhaa hiyo ofisini kwake Golioni.Picha na Mdau Othman Maulid-Zanzibar

Ramadhan: Ratiba Ya Futari Washington

|
RATIBA YA FUTARI YA PAMOJA WASHINTON DC
www.tamcousa.org

Assalam Alaykum,

Ndugu waislamu Uongozi wa Tanzanian Muslim Community in Washngton DC
Metro(TAMCO) unawakaribisha na kuwajulisha kuwa kama kwaida yetu kwa mwezi
wa Ramadhani tutakuwa tukifuturu pamoja jumammosi na jumapili zote za Mwezi wa
Ramadhani.

Tunaombwa tuudhurie na tuwajulishe wengine wote:

SAT. 08/06/11 – Sligo Avenue Neighborhood Park

Adress:
500 Sligo Avenue, Silver Spring, MD 20910

XXXXXXXX

SUN.08/07/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park
SAT.08/13/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park
SUN.08/14/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park
SAT.08/20/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park
SUN.08/21/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park
SAT.08/27/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park
SUN.08/28/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park

Address:
Hillandale PAB - Hillandale Local Park:
10615 New Hampshire Avenue,
Silver Spring,
MD 20903

XXXXXXX
TAMCO EID DAY: SAT. 09/05/11 – Hillandale Local Park

Starting at 4.00PM

If you experience problems locating the address,
Please contact TAMCO Leadership.
At
uongozi@tamcousa.org OR

Tamcotuwasiliane-owner@yahoogroups.com

Wenu
Mwenyekiti
Iddi Sandaly
301-613-5165

Thursday, July 21, 2011

Tanzania Na Afrika Kusini Zatiliana Saini Mkataba Wa Ushirikiano Kiutamaduni

Waziri wa Habari,Utamaduni na michezo Dr.Emmanuel Nchimbi na Mwenyeji wake Waziri wa Utamaduni wa Afrika ya Kusini Paul Mashatile wakisaini mkataba wa kuanzishwa rasmi ushirikiano katika Nyanja ya utamaduni kati ya Afrika ya kusini na Tanzania jana jijini Pretoria huku Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Afrika ya kusini Jackob Zuma wakishuhudia...



Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika viwanja vya kumbukumbu ya mshujaa waliopigania uhuru wa Afrika ya Kusini nje kidogo ya jiji la Pretoria jana. Wapili kushoto ni Mama Salma Kikwete na watatu kulia ni mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini.Rais Kikwete yupo nchini Afrika ya Kusini kwa Ziara rasmi ya Kitaifa ya Siku mbili...

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini wakigonga glasi wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Zuma kwa heshima yake wakati wa kilele cha Ziara Rasmi ya siku mbili nchini humo(Picha Zote; Freddy Maro)

MKUU WA MKOA WA MBEYA AKUTANA NA MADEREVA TUNDUMA(BODA) KUZUNGUMZIA KUONGEZEKA KWA SIKU ZA KUSIMAMIA MAGARI MIZANI KUTOKA SIKU TANO HADI SABA

Mkuu wa mkoa wa Mbeya akifafanua jambo kwenye mkutano huo na madereva
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mwakipesile akiwa amekasirika baada ya kukutana na maswali mengine yanayoonyesha kutokukubaliana na yale wanayoshauriwa!
Uongozi wa madereva pamoja na mkuu wa mkoa katikati na kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Mbozi wakisikiliza jambo kutoka kwa madereva hao
Meneja wa TRA kitengo cha forodha bwana Rogacian Shirima akizungumzia kuongeza idadi ya siku za kusimamia magari hayo kutoka Dar hadi Tunduma ama Kasumulu ambapo watachukua siku saba badala ya siku tano za awali.
Kamanda wa polisi wilaya ya Mbozi Afande Ernest Dudu akizungumzia utaratibu Trafiki kukagua magari hayo tu pale yanapokuwa mizani.
Hapa viongozi wa madereva wa Magari ya biashara wakikataa hivi hivi pale hoja yao ilipokumbana na upinzani wa wale wanaowaongoza.Chanzo ni mbeyayetu.blogspot.com

Wednesday, July 20, 2011

Video ya wasanii inayohusiana na Sherehe za Miaka 50 ya Uhuru Tanzania Yazinduliwa leo Jijini Dar es Salaam


Mwenyekiti wa chama cha Wanamuziki,Tanzania Flava Unit akizungumza mapema leo kuhusiana na uzinduzi wa video ya miaka 50 ya uhuru wa sanaa ya Muziki,video hiyo imefanywa na kampuni ya Visual Lab,ina jumla ya dakika zisizozidi nne ili watazamaji wasichoke, na ina wasanii zaidi ya 50 huku walioingiza sauti wakiwa 36. Watayarishaji wa Audio ni Marco Challi na Lamar, wakati video imefanywa na Adam Juma wa Visual Lab.
Msemaji Mkuu wa Tanzania Flava Unit,Mkubwa Fella akiwatambulisha viongozi waandamini wa chama hicho,mapema leo kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.kushoto kabisa ni Mjumbe wa chama hicho Keisha.
Msemaji mkuuu wa chama cha Tanzania Flava Unit,Mkubwa Said Fella akiendelea kuwatambulisha viongozi wa chama hicho,shoto kabisa ni Mjumbe Banana Zorro,Prodyuza wa Chama hicho Lamar Niekamp kutoka Fish Crub,Katibu Kalla Pina na anaefuata kushoto ni Khalid Mohamed ambaye ni Mwenyekiti Msaidizi wa Tanzania Flava Unit.
Baadhi ya Waandishi wa habari pamoja na wadau wengeine wakiangalia 'DEMO' ya video hiyo iliyozinduliwa leo kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.
Ndugu zangu habari za mchana,

Nachukua fursa hii kuwakaribisha katika uzinduzi wa video ya wasanii inayohusiana na sherehe za miaka 50 tya uhuru wa Tanzania, hii ni sehemu yetu na sisi ya kusherehekea kama vijana tukionesha kuguswa kwetu na hili, na wakati huo huo tukijaribu kuonesha mchango wetu kama vijana kwa serikali yetu ambayo kwa njia moja ama nyingine inahitaji shukrani, kwani ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo.

Tuna uhuru, tuna amani na mambo yanaenda ingawa matatizo ya hapa na pale yapo, lakini tumeangalia upande mzuri zaidi na tumeona kabisa huu ndio muda muafaka wa kukumbushana pale tuilipojikwaa, ili tupate kwernda kwa mwendo mzuri.

Katika miaka hii 50 ya Uhuru sanaa ya muziki ni moja kati ya sekta ambazo zimeleta ajira kwa vijana. Unaweza kuona jinsi wasanii mbali mbali walivyojikwamua kupitia muziki, mifano hai imo hata humu ndani, watu wanaendesha magari, watu wanaishi kwenye nyumba nzuri na wana miradi yao kupitia muziki huu wa kizazi kipya.

Si vibaya basi kwa kile kidogo unachokipata kukitolea shukrani, kuonesha kwamba unakithamini, sisi twajivunia miaka 50 ya uhuru na tunahisi kwamba tuna kila haja ya kusherehekea.

Sisi kama Tanzania Flava Unit, vijana ambao tuko katika sekta ya muziki tuliojikusanya kwa lengo la kuufikisha muziki wetu katika eneo jingine kimaudhui tumepania kufanya matamasha mengi tu nchi nzima, katika kusherehekea hili na yote haya yatakuwa ya wazi, na tutakuwa tukitoa burudani kwa watanzania, tukisherehekea nao pamoja miaka hii 50.

Kwa fikra zetu hii ni muhimu, kuna wakati mtanzania anahitaji burudani na hawezi kuingia sehemu kulipa wala hawezi kufika mahali mbali kabisa akaniona ama mimi, au Chegge ama temba, kwa nini tusimfikie na kumpa burudani?
Hilo lilikuwa wazo la kwanza.

Lakini jingine ni kwamba kuna wakati mtanzania anahitaji kuburudika, kashafikiria sana mfumuko wa bei, kafikiria sana suala la umeme ambalo linatusumbua wengi na kafikiria sana ugumu wa maisha, na mwisho wa siku akitoka nje katika uwanja wa karibu anapata burudani angalau anachangamsha ubongo wake na kuanza kujua kesho atakabiliana vipi na ugumu huu wa maisha ambao kila kukicha tunajitahidi kuhakikisha kwamba tufike sehemu, ila mtu apate unafuu.
Tuko katika hatua za mwisho kabisa kupata udhamini wa kufanya matamasha haya, na tukiwa tayari tutawafahamisha.

Video hii imefanywa na kampuni ya Visual Lab, ina jumla ya Dakika zisizozidi nne ili msichoke, na ina wasanii zaidi ya 50 huku walioingiza sauti wakiwa 36.

Watayarishaji wa Audio ni Marco Challi na Lamar, wakati video imefanywa na Adam Juma wa Visual Lab.
Hili ndio kubwa kwa leo kaka na dada zangu iwapo kuna la ziada tutaambiana!

Hamis Mwinjuma.
Mkurugenzi
Tanzania Flava Unit

GARI LA UKWELI TOKA VAM GENERAL SUPPLY ...

Hili ni Gari linapatikana Vam General Supply Co.Ltd.Nimaalumu kwa kukodisha kwa ajili ya Maharusi na Sherehe Mbalimbali kama kuna Mtu yeyote atahitaji.Ni vema ukafika katika Ofisi za Vam na Kupata Maelekezo zaidi.

VAM GENERAL SUPPLY COMPANY LIMITED

vam general supply co.Ltd, ni kampuni inayotoa huduma ya umeme,kwa watanzania wote wanao hitaji huduma safi ya vifaa vya umeme na inatoa uhakika katika vifaa vya umeme.Ni vema ukafika na kupata huduma nzuri.Wapo Mtaa wa Lumumba na Narung'ombe

TANZANIA WINS THE BAE PAYMENT ARGUMENT IN THE HOUSE OF COMMONS IN LONDON

From Second Left Hon John cheyo MP,Mussa Zungu MP, Mrs Kariuki MP and Hugh Bailey MP in the house of commons today
--
By Ayoub mzee-London
International Development Committee questioned DFID, MOJ, The Serious Fraud office and BAE Systems on Financial Crimes today in committee Committee Room 8, The Palace of Westminster. The Committee took evidence from:
At 10.00
  • Philip Bramwell, Group General Counsel, BAE Systems PLC
  • Bob Keen, Head of Government Relations, BAE Systems PLC
  • Lord Cairns, Independent Chair, BAE Systems PLC Advisory Board on Tanzania
At 10.45
  • Richard Alderman, Director, Serious Fraud Office
At 11.30
  • Rt Hon Alan Duncan, Minister of State, Department for International Development
  • Rt Hon Lord McNally, Minister of State, Ministry of Justice
  • Phil Mason, Head, Anti- Corruption, Department for International Development
  • Joy Hutcheon, Acting Director General, Department for International Development
  • Tim Jewell, Deputy Director, Criminal Law Team, Legal Directorate, Ministry of Justice
This was a one-off evidence session with two broad aims.
The first and second panels examined the background to the agreement between BAE Systems and the Serious Fraud Office arising from the criminal offence of improper book keeping, which BAE Systems admitted in connection with the sale of a military Air Traffic Control system to the government of Tanzania. The panels also addressed the issue of how the people of Tanzania will benefit from the reparations that BAE Systems has agreed to pay.
The third panel examined the BAE Systems and Tanzania case as well as whether the case allows any general lessons to be drawn about how best to combat financial crimes, including bribery, in developing countries.

The session also went on to look at the working of the Bribery Act and the Government’s guidance.
The UK parliamentary committee which comprised of Malcom Bruce MP (Chair lib Dems ),Hugh Bailey MP (Labour )Richard Burden(Labour), Sam Gyimah (Conservatives),Richard Hamington Mp (Conservatives),Pauline Latham (conservatives) Jeremy Lefroy MP( conservatives) ,Michael Maccann MP(conservatives)Anas SarwarMP(Labour) ,Chris white MP ( conservatives) were appalled by the fact that The $47 million that BAE has been ordered to pay to the "Tanzanian people" will be dispersed via selected NGOs, rather than to the government of Tanzania and were also amazed at the length of time BAE is taking to reach a decision.

The DFID was in the view that they have a great respect of the Tanzania parliamentary scrutiny procedures, a growing investigative journalism and government collective responsibility. DFID said that if Tanzania is good enough to account for the budgetary supplementary from the UK , then it must be good enough for the funds from BAE .Hon Alan Duncan, minister of state ,DFID concluded by saying that the only people are good enough to handle this money are the people of Tanzania through their democratically elected government
The low side of this is that the parliamentary committee has no legal powers on BAE in terms of specific performance

Tuesday, July 19, 2011

Message from the General Secretary

The General Secretary Greetings from CCT in Jesus’ name!
It is wonderful to once again testify upon the love of God, the riches of his mercy and the depth of his grace to his people. My heart is filled with joy as I look back at what God has done to us.
During the month of June we had a lot to do, of which none was thought to be easy. After struggling with our human frailties and worries we surrendered all to God, and He gracefully saw us through. We have seen him through successes and achievements during the Management and Executive Council meetings and our intervention in several national cross-cutting issues.
Hopefully we know or have just heard about the story of Nehemiah, the cup bearer who stood to build the wall. Although he and his people were short of resources – including time, still they managed. They managed because every person, men and women had put their minds to work. Moreover, they strategically worked each in the portion in front of their houses.
If we could work each in our positions; students and teachers, military and civilians, courts and prisons, peasants and executives, the government and its people, and every one of us, no wall could be too tall or too thick for us to build. If we work to transform our nation from where we are we can.
We should just stop grumbling and whining. Let us build our nation from where we are.
One thing is certain: God is with us.Source :http://cct-tz.org/

Sunday, July 17, 2011

TWANGA NA MSONDO NGOMA KUMCHANGIA NGURUMO


TWANGA PEPETA NA MSONDO KUMCHANGIA NGURUMO MATIBABU.
Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” imepanga kufanya onesho maalum kwa ajili ya kumchangia fedha za matibabu mwanamuziki mkongwe wa Bendi ya Msondo Ngoma Music Muhidin Ngurumo.
Onyesho hilo maalum linataraji kufanyika katika ukumbi wa Mango Garden uliopo Maeneo ya Kinondoni hapa Jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi tarehe 23-07-2011.
Burudani inataraji kutolewa na Twanga Pepeta yenyewe sambamba na Msondo Ngoma wenyewe na sehemu ya mapato ya onyesho hili yataenda kwa ajili ya kumchangia Mzee Ngurumo matibabu yake. Pia Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 Mary Khamis anataraji kuonesha ustadi wake katika kusakata mitindo ya Twanga Pepeta.
Sehemu kubwa ya maandalizi yamekwisha kukamilika ili kufanikisha onyesho hilo na Twanga Pepeta itatumia onyesho hilo kwa ajili ya kutangaza albamu yake mpya inayotarajiwa kutambulishwa hapo baadae mwaka huu. Nyimbo zilizomo kwenye albamu mpya ya Twanga Pepeta ni pamoja na Kauli, Kiapo cha Mapenzi, Umenivika Umasikini, Mtoto wa Mwisho, Dunia Daraja na Penzi la Shemeji.
Twanga Pepeta imeamua kuandaa onesho hilo baada ya kuguswa na kutambua mchango mkubwa katika tasnia ya muziki alioutoa Mzee Ngurumo ikiwa ni pamoja na kuwa mshauri wa karibu wa Bendi ya Twanga Pepeta ambayo wakati ikikua alikuwa akiwafunda wanamuziki wa Twanga Pepeta kwa vipindi tofauti.
ASET inapenda kuwaomba wapenzi wa Muziki wa Dansi kuhudhuria kwa wingi katika onesho hili maalum ili kumchangia Mzee Ngurumo fedha za matibabu. Kwa kuingia kwenye onesho basi utakuwa umemchangia Mzee Ngurumo matibabu na kisha utapata burudani mbili kali toka kwa Msondo Ngoma, Twanga Pepeta na Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 Mary Khamis.
Hassan Rehani.
Mratibu wa Onyesho.

Waandishi Wa Habari Watembelea Bwawa La Mtera ili Kujionea Hali Halisi Ya Maji


Mhandisi Mkuu wa Uendeshaji kutoka kituoncha kuzalisha umeme kwenye bwawa la Mtera akitoa maelezo ya jinsi mtambo wa uendeshaji wa umeme unavyofanya kazi kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiangalia jinsi bwawa la Mtera ilivyopungua maji.
Mhandisi Mkuu wa Uendeshaji kutoka kituo cha kuzalisha umeme kwenye bwawa la Mtera ,Julius Chomolla akionyesha kipimo cha kuonyesha maji yaliyopungua. Picha na Magreth Kinabo-MAELEZO

Saturday, July 16, 2011

JK Na Dk Bilal Waudhuria Sherehe Ya Harusi Ya Mdogo Wake JK


Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt Mohammed Gharib Bilal, wakiongozana katika Uwanja vya Ikulu Ndogo Bagamoyo wakati walipofika kuhudhuria sherehe ya ndoa ya mdogo wake na rais Kikwete, Yusuph Kikwete, iliyofungwa leo mchana katika uwanja huo na kuhudhuriwa na mbalimbali pamoja na wake za viongozi...




Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Bilala, wakiwa katika meza kuu kwenye Sherehe hiyo iliyofanyika Bagamoyo jana...


Rais Jakaya, akifurahia jambo na Mama Zakhia Bilal (kushoto) na Mam Asha Bilal (wapili kulia)
Mama Salma Kikwete (kushoto) akiwa na Mama Zakhia Bilal (katikati) na Mama Asha Bilal, wakati wakiwa katika sherehe hiyo ya ndoa ya mdogo wake na Rais Jakaya Kikwete, Yusuph Kikwete leo mjini Bagamoyo.
Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR