Friday, September 30, 2011

Jeshi latwaa uwanja wa ndege, Sirte

Picha za Gaddafi za ng'olewa uwanjani
Wanajeshi wanaoitii serikali ya mpito ya Libya wametwaa uwanja wa ndege katika mji wa Sirte, mahali alikozaliwa aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.
Wapiganaji walisonga mbele kupitia majengo ya uwanja wa ndege yaliyoharibiwa, wakiharibu miundombinu ambayo ilikuwa alama ya utawala wa Gaddafi.
Taarifa kuhusu alipo kiongozi huyo wa Libya, aliyeng'olewa madarakani, bado haijulikani lakini wengi wa wanafamilia wake wamekwisha kimbia kutoka Libya.
Mtoto wake wa kiume Saadi yuko nchini Niger. Saa kadha baada ya hati ya kumkamata kutolewa, waziri mkuu wa Niger amesema Saadi hatarejeshwa nchini Libya.
Taarifa ya Shirika la Polisi la Kimataifa, Interpol, ya kukamatwa kwa Saadi Gaddafi, inasema anatakiwa nchini Libya ambako anatuhumiwa kujipatia mali kimabavu na kutumia vitisho vya kijeshi wakati alipokuwa kiongozi wa Shirikisho la Kandanda la Libya.
Interpol imesema akiwa kamanda wa vikosi vya kijeshi, anatuhumiwa kuhusika katika ghasia dhidi ya raia wakati wa maasi, pia anakabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Mataifa, vikiwezo vya usafiri na kukamatwa mali zake.
Interpol imesema Saadi kwa mara ya mwisho alionekana nchini Niger na kuziomba nchi wanachama kusaidia kubaini alipo na kumrejesha Libya.
Lakini akizungumza nchini Ufaransa, Waziri Mkuu wa Niger Brigi Rafini amesema Saadi Gaddafi uko salama na "yuko katika mikono ya serikali ya Niger" katika mji mkuu Niamey.
"Kwa sasa, hakuna suala la yeye kupelekwa Libya" Bwana Rafini ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, akisema hatatendewa haki ya kimahakama akipelekwa huko.
Interpol tayari imetoa hati ya kukamatwa kwa Kanali Gaddafi na mtoto wake mwingine wa kiume, Saif al-Islam.
Wapiganaji watiifu kwa Gaddafi wamekuwa wakiweka upinzani mkali katika mji wa Sirte tangu askari wanaowaunga mkono wapiganaji wa Baraza la Taifa la Mpito la Libya (NTC) waanze mashambulio yao katika mji huo.
Majengo mawili ya viongozi Mashuhuri katika uwanja wa ndege wa Sirte ni ya kifahari, yakidhihirisha mji wa nyumbani kwa Muammar Gaddafi - yakiwa yamewekewa skrini kubwa za Televisheni, bafu ya mvuke au Sauna na kitanda kikubwa.
Wapiganaji vijana waliegesha bunduki zao katika viti vilivyonakishiwa kwa dhahabu, wakitaniana na kufurahia madaraka ya ghafla waliyoyapata - wachache kati yao wamewahi kuuona mji wa Sirte hapo kabla, achilia mbali mazingira ya kifahari aliyoishi kiongozi wao.

uharibifu

Malori yaliyochorwa chorwa rangi yaliharibiwa katika barabara ya lami, wakilenga ngome ya majeshi ya Gaddafi katika upande wa pili wa barabara ya kurukia na kutua ndege.
Wiki mbili zilizopita, majeshi ya NTC yaliutwaa uwanja wa ndege, umbali mfupi kutoka katikati ya mji, lakini wakarudishwa nyuma na wanajeshi wanaomtii Gaddafi.
Mwandishi wa BBC, Jonathan Head anasema wakati huu majeshi ya NTC yana matumaini ya kuutwaa kabisa uwanja huo wa ndege, mbali na kukabiliwa na mashambulio ya maroketi na bunduki kutoka upande wa pili wa njia ya kurukia na kutua ndege.
Uwanja wa ndege upo umbali wa kilomita 5 (maili 3) kutoka mjini Sirte.
Majeshi ya Baraza la Mpito la Taifa la Libya (NTC) hivi karibuni pia yalitwaa bandari ya Sirte.

Makabiliano makali

Mapigano makali yameripotiwa kuendelea Alhamisi, kwa pande zote mbili wakishambuliana kwa silaha nzito za kivita.
Ndege za Nato zimekuwa zikiendesha mashambulio ya anga dhidi ya vituo vya kijeshi yakiwemo maghala ya kuhifadhi silaha na risasi.
Miji ya Sirte na Bani Walid ni maeneo makubwa ya mwisho ambayo yako chini ya udhibiti wa wafuasi wa Gaddafi, na miji yote miwili imeshuhudia mapigano makali katika siku za karibuni.

Gaddafi na familia

Maafisa wa NTC wanasema wanaamini kuwa Kanali Gaddafi huenda anajificha katika jangwa kusini mwa Libya.
Wanasema mmoja wa watoto wake wa kiume, Mutassim, huenda yuko Sirte, na mwingine, Saif al-Islam, yuko Bani Walid.
Mke wa Kanali Gaddafi na watoto wake watatu walikimbilia Algeria mwezi uliopita. Na watu wengine wa familia ya Gaddafi walikwenda Niger.Chanzo ni bbckiswahili

Thursday, September 29, 2011

ZFA CHAILILIA SERIKALI KUHUSU UDHAMINI WA LIGI KUU



Na Hamad Hija-Maelezo Zanzibar
KATIBUmsaidizi wa chama cha soka cha Zanzibar ZFA Masuod Attai ameiomba Serikali ya Mapinduzi kuzungumza na taasisi na kampuni mbali mbali nchini ili ziweze kudhamini ligi kuu ya Zanzibar.
Masuod Attai alitoa ombi hilo mbele ya Kamati ya Mifugo, Uwezashaji, Habari na utalii ambapo kamati hiyo ilikuwa ikizungumza na viongozi wa vyama vya michezo vya Zanzibar
Amesema kuwa kuna haja kubwa kwa Serikali kuzungumza na makampuni hayo ili kuweza kusaidia kudhamini ligi kuu ya Zanzibar ambayo kwa sasa haina mdhamini.
Akitaja makampuni ambayo Serikali inaweza kuzungumza nayo nakuweza kusaidia, ni pamoja na Kampuni ya Simu ya Vodacom, Zantel, Tigo na Air tel ambapo kampuni hizi zinauwezo wa kusaidia katika masuala mengi yakiwemo ya michezo
Amesema msimu wa mwaka 2008-9 Zantel ilikuwa mdhamini mkuu wa ligi hiyo ambapo kwa sasa wamewaacha mkono hivyo Serikali ni vyema izungumze na makampuni ambayo yapo Nchini ili kuiokoa ligi hiyo.
Amefahamisha kuwa licha ya kuwa na udhamini wa million 120 msimu wa 2008-9 ambazo zilikuwa hazikidhi haja lakini uliweza kusukuma mbele ligi hiyo jambo ambalo kwa sasa limekosekana kabisa
Attai amesema kuendesha ligi kwa msimu mmoja kunagharimu pesa nyingi katika kuendesha na kwa sasa chama cha soka cha Zanzibar hakina pesa hizo kwa ajili ya kugharamia ligi hiyo.
Mbali na kuiomba serikali kufanya hivyo pia Katibu huyo msaidizi wa chama cha soka cha zanzibar ameiomba Serikali kuzisaidia timu ambazo zinawakilisha Nchi katika michezo ya kimataifa.
Amesema kucheza mechi moja kwa timu inalazimu kutumia jula ya shilingi 30milion hivyo Serikali inawajibu mkubwa kuvisaidia vilabu vyetu ili viweze kushiriki kikamilifu katika mashindano yanayovikabili vilabu hivyo.

Wednesday, September 28, 2011

HILI HAPA DUDE LA CHADEMA HUKO IGUNGA !



MBILI ZA CCM ZASHINDWA KUTUA ZABAKI KIA, YA  CUF KUPASUA ANGA LEO 
Waandishi Wetu, Igunga
WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilitikisa anga la Igunga baada ya kuanza kutumia helikopta kufanya kampeni zake, zile mbili za wapinzani wao, CCM zikishindwa kuwasili jimboni humo na kubaki Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutokana na sababu za kiufundi.Wakati Chadema ikipasua anga na mbili za CCM zikibaki KIA, helikopta ya Chama cha Wananchi (CUF) nayo imeshindwa kutua Igunga jana na sasa inatarajiwa hapa leo.

Helikopta ya Chadema ilianza kuonekana katika anga la Igunga saa 10:40 jioni ikiwa na maandishi makubwa ya chama hicho na rangi ya bluu.Ujio wa helikopta hiyo ulivuta kwa muda idadi kubwa ya wananchi waliokuwa kwenye Viwanja vya Sabasaba wakisubiri ujio wa helikopta mbili za CCM, ambazo awali, ilielezwa kuwa zingewasili saa 8:00 mchana.

Baadaye ilielezwa kwamba helikopta hizo za CCM zingetua Igunga saa 11:30 jioni zikiwa na makada wa chama hicho akiwamo Katibu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.

Hata hivyo, ilipofika saa 12:00 jioni, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akitumia gari la matangazo la Bendi ya muziki ya ToT Plus alitangaza kwamba helikopta hizo zisingeweza kutua Igunga kutokana na sababu za kiufundi.
Alisema zilichelewa kupata vibali kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam na kwamba baada ya kutua KIA ilishauriwa kuwa ni vyema zilale hapo.

Alisema kama helikopta hizo zingeondoka KIA jana jioni na kufika hapa usiku wakati tayari kungekuwa na giza kitu ambacho kisingekuwa kizuri kiusalama. Alisema helikopta hizo sasa zitawasili leo saa 4:00 asubuhi.

Matumizi hayo ya helikopta yanawafanya wananchi wa Igunga kushuhudia kampeni nzito na za aina yake tangu kufanyika kwa uchaguzi wa kwanza wa vyama hivyo mwaka 1994 na Rostam Aziz kushinda.Jimbo hilo lenye wapiga kura 170,000 katika vijiji 96, halijawahi kushuhudia kampeni nzito kiasi hicho zinazohanikizwa na magari yenye vifaa vya kisasa vya muziki.

Habari kutoka ndani ya CCM, zinaeleza kuwa katika kujihakikishia kura katika kipindi hiki cha lala salama, chama hicho kitawatumia makada wake, Makamba na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli wanaoelezwa kuwa na ushawishi mkubwa.

Kulingana na vyanzo mbalimbali vya habari, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CCM anatarajiwa kurudi tena hapa keshokutwa.Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye aliwasili hapa jana kuongeza nguvu kwa viongozi wa chama hicho ambacho idadi kubwa ya wabunge wake wameweka kambi hapa.

Helikopta ya CUF
Kwa upande wake, CUF kinatarajiwa kuanza kutumia helikopta yake kuanzia leo huku Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Juma Duni Haji akitarajiwa kufunga pazia la kampeni za chama hicho ambazo, awali zilitarajiwa kufungwa na Katibu Mkuu wake ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad.

Akizungumzia na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema kampeni hizo sasa zitafungwa na Haji anayetarajia kuwasili wakati wowote katika kipindi hiki cha mwisho wa kampeni.Mtatiro alisema tayari wabunge wa chama hicho  akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar) Ismail Jussa wanaendelea na kampeni jimboni humo.

CCM, Chadema vyatuhumiana
Kiwewe cha uchaguzi huo kimezidi kutesa vyama vya CCM na Chadema, baada ya kuendelea kutuhumiana huku chama tawala kikidai kunasa kile ilichokiita mpango wa siri wa wapinzani wake hao wa kujitangazia ushindi kabla Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kufanya hivyo.

Chadema nacho kimekituhumu CCM kwamba kimeandaa mpango wa kupeleka wapigakura mamluki kutoka katika baadhi ya mikoa ukiwamo Dar es Salaam.

Jana, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wassira aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa kwamba Chadema kimepanga mpango huo wenye lengo la kuwaandaa wanachama wake waone wameibiwa kura pindi CCM kitakapotangazwa mshindi.“Tunazo taarifa za uhakika kuwa wamepanga kutumia magari ya matangazo kutangaza kuwa Chadema imeshinda, hata kabla ya kura kuhesabiwa ili wapate leseni ya kuanzisha vurugu,” alisema Wassira.

Wassira ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano), alisema tayari CCM wameviarifu vyombo vya ulinzi na usalama ili kuchukua hatua na pia kuwaelimisha na kuwasihi wananchi kutoingia katika mtego huo.

“Lengo ni kuwaharibu vijana kisaikolojia kwamba yakitangazwa matokeo tofauti waone wamechakachuliwa kura zao na CCM. Tunawasihi Chadema na wanachama wao watulie wakati wananyolewa,” alisema Wassira.

Wassira alisema wanakusudia kutumia mikutano ya hadhara ya kampeni iliyobakia wiki hii ya lala salama, kuwaeleza wananchi juu ya mpango huo wa Chadema ambao alidai hauwatakii mema wananchi wa Igunga.

Hata hivyo, Mratibu wa Kampeni za Chadema  Igunga, Mwita Waitara alikanusha vikali madai hayo akisema hawana sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa wananchi wameshafanya uamuzi wa kuikataa CCM.“Wassira anafahamu utaratibu wa kutangaza matokeo ulivyo kwamba Chadema hatuna uwezo huo. Hivi kama tulikuwa na uwezo huo kulikuwa na sababu gani ya kufanya kampeni na kuteua hadi mawakala?,” alihoji.

Alikishutumu CCM akidai kuwa kina mpango wa kuingiza watu 1,050 kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Singida na Shinyanga ili watumie shahada bandia kukipigia kura chama hicho tawala.Waitara alidai kuwa watu 500 watatoka Dar es Salaam, 300 Singida na 250 Shinyanga lakini akasisitiza kuwa Chadema kina mtandao mpana na kitahakikisha kinazuia mpango huo usifanikiwe.

Chagonja atua Igunga

Kamishina wa Polisi anayeshughulikia Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja jana aliwasili hapa na kusema polisi watakabiliana na yeyote atakayejaribu kuanzisha vurugu.“Nasema vurugu sasa basi na ninaonya yeyote atakayejaribu kutuchokoza tutakabiliana naye kwa nguvu zote… wananchi waende kwa uhuru vituoni kupiga kura,” alisema.

Kwa upande wake, Naibu Kamishina wa Polisi anayeratibu usalama Igunga, Isaya Mngulu amesema polisi wamefungua vituo tisa kwa ajili ya kukabiliana na matukio ya vurugu yatakayojitokeza.

Alisema vituo hivyo vina vifaa vyote vya kisasa yakiwamo mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha na kwamba vikosi vimejizatiti kukabiliana na hali yoyote ya vurugu itakayojitokeza.

Alivitaja vituo hivyo kuwa vipo katika maeneo ya Simbo, Mwisi, Nkinga, Sungwisi, Ziba, Mwanshimba na Itumba na kwamba kila kituo kina polisi wa kutosha wenye uzoefu wa kukabiliana na kila aina ya vurugu.

Katika kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika kwa amani na usalama, askari mgambo 325, Magereza wanane na polisi 94 watatumika katika kusimamia zoezi la upigaji kura katika vituo vyote 427.

Maandalizi yakamilika
Msimamizi wa Uchaguzi Igunga, Protas Magayane alisema jana kwamba vifaa vyote kwa ajili ya upigaji kura vipo tayari na vitaanza kusambazwa katika vituo vyote Jumamosi.

Magayane alisema orodha ya wapiga kura itabandikwa vituo kesho Alhamisi na kuwataka wale wote waliojiandikisha waende kuhakikisha majina yao na kufahamu vituo watakavyotumia kupiga kura.

Alisema wasimamizi wa vituo vya uchaguzi wapatao 427 waliapishwa jana na kwamba NEC itafanya kikao na viongozi wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo ili kuwekana sawa.

CUF nayo yapata homa
CUF nacho kimetoa shutuma mbalimbali dhidi ya CCM ikiwamo ya kuingiza makontena ya sukari wilayani Igunga kwa lengo la kugawa kwa wananchi kama njia ya kurubuni wananchi wakipigie kura.
 
Tuhuma nyingine za CUF kwa CCM ni kuwa  kinatarajia kuingiza kundi la makomandoo waliomaliza mafunzo na semina katika Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwatisha wapiga kura siku za mwisho za kampeni na uchaguzi.

Tuhuma hizo zilitolewa jana Mtatiro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.
 
Alisema tayari chama hicho kimepata taarifa za kuaminika kuwa kuna makontena yanayotarajia kusafirishwa kutoka Mara kwenda Igunga kwa ajili ya kugawanywa kwa wapiga kura. Bila kutaja kiasi alisema zinatarajiwa kuingia Septemba 29.

“Hii ni rushwa, haiwezekani kipindi hiki cha uchaguzi Serikali ya CCM kuleta kontena za sukari... tunataka Igunga ipate mbunge halali atakayechaguliwa na wananchi na sisi tumejipanga kuzuia jaribio hilo,” alisema Mtatiro.
 
Pia alidai kwamba chama hicho kimepanga kugawa chakula cha msaada nyumba kwa nyumba siku moja kabla ya kupiga kura na kwamba mpango huo umekamilika na magari yameandaliwa kufanya kazi hiyo Septemba 31 na Oktoba Mosi.

Akijibu tuhuma hizo Mratibu wa Kampeni wa CCM, Mwigulu Nchemba alikanusha na kusema wapinzani wao hao wana maralia ya uchaguzi.
 
Nchemba alisema kambi inayodaiwa ilifanyika siku nyingi na shughuli zake ziliisha... “Kambi tulishamaliza na sasa hakuna kinachoendelea, CCM hatuna mpango wa kuingiza vijana katika mji huu kutoka nje kwa ajili ya uchaguzi.”

Kuhusu chakula alisema Serikali imekuwa ikigawa chakula cha msaada katika maeneo mbalimbali yenye njaa na ilianza kufanya kazi hiyo kabla ya uchaguzi.

“Wanasema tunataka kugawa chakula Septemba 31 na Oktoba Mosi hapa Igunga? Siyo kweli kama tunafanya hivyo kwa ajili ya uchaguzi. Serikali inagawa chakula cha msaada katika maeneo yote ya njaa ikiwamo Igunga” alisema Nchemba.Chanzo: Mwananchi.

Tuesday, September 27, 2011

Silaha kudhibitiwa Libya

Mahmoud Jibril
Mahmoud Jibril waziri mkuu wa serikali ya mpito nchini Libya
Afisa wa Umoja wa Mataifa wa ngazi ya juu wa masuala ya kisiasa ameonya kuhusu hatari kutokana na silaha za kemikali nchini Libya.
Afisa huyo, Lyn Pascoe, alikuwa akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, uliohudhuriwa na waziri mkuu wa mpito wa Libya Mahmoud Jibril.
Bw Pascoe amesema mabadiliko ya haraka yanayofanyika nchini Libya yameongeza wasiwasi kuhusu usalama wa silaha za kemikali.
Amebainisha kwamba shughuli ya kuziteketeza silaha ilisitishwa mwezi Februari wakati harakati za mapinduzi zilipoanza na kundi la kimataifa la ukaguzi wa silaha lilipoondoka nchini humo.

Silah zikusanywe

Waziri mkuu wa mpito wa Libya Mahmoud Jibril ameelezea umuhimu wa silaha zilizotapakaa nchini humo kukusanywa haraka, siyo tu nchini Libya bali hata nje ya mipaka ya nchi hiyo.
Lakini amesisitiza tena kwamba serikali yake haingeweza kutekeleza hilo au kukamilisha majukumu yake hadi hapo Umoja wa Mataifa utakapoziachilia mali zote za Libya zinazoshikiliwa tangu kuzuka kwa mgogoro nchini humo, wakati Muammar Gaddafi alipokuwa bado madarakani.
Mpaka sasa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelegeza baadhi tu ya vikwazo dhidi ya Libya.Chanzo ni bbckiswahili.com

Monday, September 26, 2011

IMBA, MTIBWA ZAINGIZA MIL 74/-

S

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Mtibwa Sugar iliyochezwa Septemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 74,345,000.
Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 13,285 ambapo kiingilio kilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 7,000 rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B na sh. 20,000 kwa VIP A.
Eneo lililoingiza watazamaji wengi ni kwenye viti vya bluu na kijani ambapo waliingia 11,798 wakati lililoingiza watazamaji wachache ni la VIP A ambapo waliingia 58.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo ambazo ni sh. 11,637,000 na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 11,340,762.70 kila timu ilipata sh. 15,410,171.19.
Mgawo mwingine ulikwenda kwa gharama za mchezo (sh. 5,136,723.73), uwanja (sh. 5,136,723.73), TFF (sh. 5,136,723.73), Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF (sh. 2,568,361.86), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam- DRFA (sh. 2,054,689.49) na Baraza la Michezo la Taifa- BMT (sh. 513,672.37).Chanzo ni fullshangweblog

Sunday, September 25, 2011

Maeneo Ya Wazi Kurudishwa Kwa Wananchi


NA  MAGRETH  KINABO – MAELEZO
 
   
WIZARA YA Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imejipanga kwa makini   ili kuhakikisha kuwa maeneo yote ya wazi yanarudishwa kwa wananchi ambapo matumizi yake yatakuwa kwa manufaa ya watanzania wote.
 
Aidha  wizara hiyo imesema kuwa itatoa muda maalum kwa watu wote walivamia maeneo  hayo kuondoka  wenyewe  na  utakapokwisha muda uliopangwa  itakuja kubomoa hivyo hakutakuwa na msamaha.(hakuna cha msalie mtume).
 
Kauli hiyo ilitolewa (leo)jana na Makamu Mwenyekiti  wa Kamati ya   Bunge  ya Ardhi na Maliasili na Mazingira, Abdulkarim  Shah, wakati akifunga maonesho ya  kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ya wizara hiyo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa, Mnazimmoja, jijini Dares Salaam.
 
Shah alitoa kauli hiyo ikiwa ni matazamio ya  miaka 50 ijayo ya wizara hiyo huku akisema maeneo hayo  yamepangwa kwa faida ya wananchi wote.
 
“Napenda kusisitiza kwamba  taaluma ya  upangaji miji inahitajika kutiliwa maanani na serikali haitakubali mipango hiyo kubadilishwa matumizi kiholela. Natoa rai hii kwa jamii kushirikiana na serikali kulinda maeneo ya wazi yaliyoko katika maeneo yao,” alisema Shah.
 
Aliwataka watendaji husika hasa wa halimashauri kutobalidilisha  matumizi ya ardhi .
 
Aliongeza kuwa wizara hiyo imeandaa mikakati ya kuwa na mipango shahidi ya uendelezaji miji itakayokidhi mahitaji ya idadi kubwa zaidi ya watu watakaoishi mijini.
 
Pia  kuwa na mipango itakayowezesha ujenzi wa miji nadhifu, ya kisasa na endelevu,kuzijengea uwezo halimashauri kusimamia na kudhibiti uendelezaji wa miji na kuwa na mipango ya matumizi ya ardhi kwa kila eneo la makazi nchini. 
 
“ Wizara imedhamiria kuongeza kasi ya upimaji wa ardhi nchini kwa matumizi mbalimbali pamoja na kupunguza gharama za upimaji, ambapo nchi itakuwa imejenga kituo cha kupokea na kusambaza picha za saltillite, vituo vingi zaidi cha upimaji vitajengwa,” alisema.
 
Makamu Mwenyekiti huyo  aliongeza kuwa wizara hiyo itaanza kutunza kumbukumbu za upimaji  na ramani kwa kutumia teknolojia ya kisasa, ambapo sasa inatumika  mikoa 15 baadae itakuwa mikoa yote  hadi wilayani kulingana na uwezo wa bajeti.
 
Alisema ili kuwawezesha wananchi kutumia ardhi kama mtaji  wizara itahakikisha kuwa mashamba ya wananchi vijijini kote nchini yanabainishwa yanapimwa na wamiliki wake wanapewa hatimiliki za kimila.
 
Alisema kwa upande wa Shirika la   Nyumba  la Taifa(NHC)  limejipanga kujenga nyumba 150,000 katika kipindi cha miaka 50 ijayo na kujenga nyumba kwa ubia kwa kuwashirikisha wawekezaji wengine.

Saturday, September 24, 2011

Rais Kikwete ang'ara katika ufunguzi wa mkutano wa DICOTA 2011 jijini Washington DC

 
 
Wafadhili toka taasisi mbalimbali za umma na binafsi waliofanikisha DICOTA 2011 wakipozi na Rais Kikwete na Meza kuu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernard Membe akiongea kabla ya kumkaribisha Rais Kikwete kuhutubi hadhira na kufungua rasmi mkutano wa DICOTA 2011

Friday, September 23, 2011

Rais Jakaya Kikwete Ahutubia Baraza La Umoja Wa Mataifa Nakukutana Na Kiongozi Wa Serikali ya Mpito Nchini Libya

 
Rais Jakaya Kikwete akihutubia Mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa jijini New York jana
 
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kiongozi wa serikali ya mpito ya Libya Bw. Mustafa Abdel-Jalil jijini New York Marekani ambako wote wanahudhuria mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika maongezi mafupi na kiongozi wa serikali  ya mpito ya Libya Bw. Mustafa Abdel-Jalil
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtabulisha Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mh Ombeni Sefue kwa  kiongozi wa serikali  ya mpito ya Libya Bw. Mustafa Abdel-Jalil.Picha na IKULU

Thursday, September 22, 2011

WAZIRI MKUU AKIWA TARIME


Wasanii wa Tarime wakicheza ngoma maarufu ya Eritungu wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara katika Misheni ya kanisa Katoliki ya Masanga  akiwa katika zaira ya mkoa wa Mara, Septemba 12,2011.Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Sister Maria wakati alipowasili kwenye misheni ya Kanisa katoliki ya Masanga wilayni Tarime  akiwa katika ziara ya mkoa wa Pwani Septemba 21,2011
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifungua kliniki ya mama na mtoto katika kituo cha afya cha kanisa Katoliki jimbo la Musoma cha Masanga wilayani Tarime. Alikuwa katika ziara ya mkoa huo Septemba 21,2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wednesday, September 21, 2011

Vodacom Mwanza Cycle Challenge Kufanyika Mwezi Ujao


 Meneja udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mbio za baiskeli "Vodacom Mwanza Cycle challenge"uzinduzi huo umefanyika katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga mbio hizo zitafanyika tarehe 22 mwezi wa kumi mwaka huu zikianzia shinyanga mpaka Mwanza,katikati Mwenyekiti wa chama cha baiskeli cha Mkoa wa shinyanga(Kamwashi) Elisha Eliasi,anaefuata ni katibu wa chama hicho Lukas Bupilipili...
 
 Meneja udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akionyesha nembo itakayotumika katika mashindano ya mbio za baiskeli "Vodacom Mwanza Cycle challenge 2011"zitakazoanzia Shinyanga hadi Jijini Mwanza mnamo tarehe 22 mwezi wa kumi mwaka huu.kulia Mwenyekiti wa chama cha baiskeli cha Mkoa wa shinyanga(Kamwashi) Elisha Eliasi.
.Baadhi ya waendesha baiskeli wa Mkoa wa Shinyanga wakifanya mazoezi tayari kwa kujiandaa kushiriki mashindano ya mbio za baiskeli "Vodacom Mwanza Cycle challenge 2011"zitakazoanzia Shinyanga hadi Jijini Mwanza mnamo tarehe 22 mwezi wa kumi mwaka huu.
 --
Shinyanga Septemba 21 2011,
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetangaza kuandaa na kuyadhamini mashindano ya baiskeli ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge ambayo yamekuwa yenye mvuto wa hali ya juu katika mikoa ya kanda ya ziwa.Mashindano haya yataanzia mjini Shinyanga na kumalizikia Jijini Mwanza mwezi ujao na yatagharimu zaidi ya shilingi milioni 50.

Akizungumza naWaandishi wa Habari,leo/jana, katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa alisema kwamba mashindano ya mwaka huu yameboreshwa zaidi na kuwaomba waendesha baiskeli kujitokeza kwa wingi.

“Mashindano haya yameboreshwa kwa upande wa zawadi, ubora na viwango, na tofauti na miaka ya nyuma, mashindano ya mwaka huu yatahusisha mikoa miwili muhimu kwa mchezo wa baiskeli kanda ya Ziwa, yani Shinyanga na Mwanza”Alisema.

Alisema mashindano hayo yatafanyika tarehe 22 mwezi ujao na kwamba yatakuwa mbio za kilomita 196 kwa wanaume, 80 kwa wanawake, upande wa walemavu ni Kilometa 15 kwa walemavu wanaume na Kilomita 10 kwa walemavu wanawake.

“Washindi katika kila kundi watapewa zawadi mbalimbali ambazo tutazitangaza baadae,”Alisema.

Alifafanua kuwa mashindano ya mwaka huu ya Vodacom Mwanza Cycle Challenge yameandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa takribani miaka mitano na pia Vodacom ina nia ya kuendelea kuandaa na kukuza mchezo huu ili Tanzania iweze kujulikana zaidi kimataifa katika mchezo huu wa baiskeli.


“Shindano hili la Vodacom Mwanza Cycle Challenge ni mahususi kwa kukuza mchezo huu hapa nchini kwa lengo la kupata wawakilishi bora katika mashindano mbalimbali ya kimataifa,”alifafanua.

Katika kuzingatia kuwa mwaka huu Tanganyika inasherehekea miaka 50 ya uhuru, Vodacom Tanzania itatoa zawadi ya mshiriki mwenye umri wa kuanzia miaka 50 atakaemaliza wa kwanza katika kundi la washiriki 50 wa kwanza. Hivyo amewataka Watanzania wenye uwezo kujiandikisha kwa wingi ili kuweza kushiriki na hatimae kujishindia zawadi kem kem
Nae Mwenyekiti wa Baiskeli Kanda ya Ziwa bwana Elisha Eliya, amesema mwaka huu ili kuleta mabadiliko na kuboresha zaidi mashindano haya, mbio zitaanzia Mkoa wa Shinyanga na kumalizikia Mwanza kwa sababu hii ni mikoa miwili inayoongoza katika uendeshaji wa baiskeli katika kanda hii.

Amewataka wanamichezo wote nchini wanaoshiriki katika mashindano haya kuanza kujiandaa wao pamoja na vifaa vyao vya michezo ili waweze kuwa katika hali nzuri ya kiushindani zaidi.
Ametoa wito kwa washiriki kutoka mikoa yote nchini kujiandikisha kwa wingi na kufika Shinyanga mapema ili kuhudhuria semina ya washiriki wote siku moja kabla ya mashindano.

Bwana Eliya amesema kuwa mashindano ya mwaka huu yatakuwa na ushindani wa hali ya juu kwani njia itakuwa ya moja kwa moja na watahakikisha hakuna mtu atakaeingia kwenye mashindano kati kati ya njia hivyo kupata washindi halali,Na alichukua frusa hiyo kwa kutoa wito kwa makambuni mbalimbali hapa nchini kujitokeza kudhamini mbio hizo.


Vodacom Tanzania imekuwa ikidhamini michezo mbalimbali kama vile Soka, Riadha, kuogelea, mashindano ya boti, mashindano ya Mbuzi, Vodacom Miss Tanzania, Tenisi na mingine mingi ili kuhakikisha kwamba taifa linafanya vizuri katika tasnia nzima ya michezo.

Makamu Wa Rais Akutana Na Mwakilishi Maalum Wa Katibu Mkuu Umoja Wa Mataifa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Marta Santos Pais, Mwakilishi maalum wa Katibu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na harakati za kutokomeza unyanyasaji wa watoto, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ripoti ya unyanyasaji wa watoto inayohusu hali ya Tanzania na inayotarajiwa kuwasilishwa rasmi hivi karibuni (Jumanne, Septemba 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR).

Tuesday, September 20, 2011

MAMBO YANAKWENDA !

 Kushoto ni Baunsa MKuu wa Mzalendo Pub aitwae Rashindi akiwa na mimi Victor Mombeki kwenye sakafu ya ukumbi huo siku ya Jumamosi usiku ambapo tulichangamka sana , hapo chini ni kijana Mujauzi akivuta raha kwa sana na ...

Monday, September 19, 2011

JK In America


1. President Jakaya Kikwete delivers his keynote address at the launch of the Africans Leaders against Malaria (Alma) Scorecard for accountability and action at the Sentry Center in New york. Others from left are Ms Obiageli “Oby” Ezekwesili, the World bank  Vice President for the Africa Region, Minister for Health of Rwanda Dr  Agnes Binaguaho, Professor Awa Marie Coll-Seck, the Roll Back Malaria Partnership Executive Director, and Mr Raymond G. Chambers, the UN Special Envoy for Malaria. (Ikulu Photo)

2: President Jakaya Kikwete speaks during a panel discussion on women and Agriculture: A Conversation on improving Global Food security organised on Monday the US Secretary of State Mrs Hilary Clinton (seated right) at the Intercontinental hotel in New York. (IKulu Photo)

Wanaume waingia Ubalozini Uingereza...

Chege na Temba wakiwa na ofisa wetu Ambokile katika ofisi ya uhamiaji .JPGChege na Temba wakiwa na ofisa wetu Ambokile katika ofisi ya uhamiaji.
 
 
Salam,

URBAN PULSE CREATIVE na Miss Jestina Blog wanakuletea Ziara ya Wanaume kutoka kundi la  TMK wakiwalishwa na Mh Temba na Chege walipopata fursa ya kutembelea Ubalozi wetu hapa mjini London kabla ya kumaliza show zao hapa nchini Uingereza siku chache zilizopita. Vilevile waliweza  kutembelea idara mbalimbali na kujionea jinsi gani Ubalozi wetu hapa London unavyofanya kazi hususani  katika idara nyeti ya Uhamiaji inayoongozwa na ofisa Ambokile na Kupiga Picha za pamoja wakiwa na  Mh Naibu Balozi Mh Chabaka Kilumanga Pamoja  na baadhi ya maofisa wa Ubalozi.
Baada ya Ziara yao Freddy Mtoi Kutoka BBC alifanya nao mahojiano maalum  ndani ya ubalozi na yatarushwa hewani  duniani kote.
Asanteni,
 Ziara hii iliandaliwa na Urban Pulse pamoja na miss Jestina Blog Ikishirikiana na Ubalozi wetu

Saturday, September 17, 2011

Wabunge Chadema Wafikishwa Polisi



JESHI la Polisi wilayani Igunga limefungua majalada mawili na kuwahoji watu watano wakiwamo wabunge wawili wa Chadema; Suzan Kiwanga na Sylvester Kasulumbayi, kwa vurugu zilizotokea juzi, kufuatia Mkuu wa Wilaya hiyo, Fatma Kimario, kukamatwa na makada wa chama hicho. Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na viongozi wa Chadema zimeeleza kuwa, wabunge hao walihojiwa kwa nyakati tofauti jana katika Kituo cha Polisi cha Igunga wakiwa na mwanachama mmoja wa chama hicho,  Anuari Kashaga.

Mkuu wa kitengo cha ufuatiliaji wa tathimini kutoka Makao Makuu ya Upelelezi wa makosa ya jinai, Issaya Mungulu, alieleza kuwa polisi imewashikilia watu sita na kufungua majalada mawili kituoni hapo kuhusu shambulio la aibu na kuingiliwa kwa ratiba ya mkutano wa kampeni.

Jalada moja ni la Mkuu wa Wilaya kunyanyaswa na kufanyiwa shambulio la aibu na la pili na Chadema wanaodai kuwa ratiba yao iliingiliwa na Mkuu huyo wa Wilaya na kwa lengo la kuvuruga mkutano wao wa kampeni  uliokuwa unafanyika katika eneo hilo

Alisema Chadema walitakiwa kufanya mkutano katika eneo hilo kuanzia saa 4 asubuhi juzi hadi saa 6 mchana na wakati huo huo mkuu wa Wilaya alikuwa akifanya mkutano wa ndani na watendaji wa Serikali.

“Kufuatia mkutano huo wa mkuu wa Wilaya kuingiliana na Chadema eneo hilo, wanachama, viongozi, wafuasi na wapenzi wao, walichukizwa na hali hiyo wakidai kuwa wameingiliwa kwenye mkutano wao na Mkuu huyo wa Wilaya,” alisema Mungulu.

Aliongeza kuwa: “Kwa pamoja waliamua kuvamia kikao cha Mkuu wa Wilaya kwa nia ya kumshambulia na kuvunja kikao alichokuwa akikiendesha.”

Alisema kuwa katika tukio hilo Mkuu wa Wilaya alivuliwa hijabu, viatu, alikatiwa mkufu ambao thamani yake haijajulikana na simu yake ya mkononi aina ya Sumsung yenye thamani ya Sh400,000 ilipotea. “Pia walimtukana matusi mbalimbali ya kumdhalilisha,” alisema.
Alisema jeshi la polisi lilipokea taarifa hizo kutoka kwa Afisa Tawala wa Wilaya aitwaye, Sumera Manoti na baadaye kuzipokea kutoka kwa askari walikwenda eneo la tukio kwa lengo la kukabili vurugu, kurudisha hali ya amani na kukagua eneo la tukio kwa nia ya kukusanya vielelezo na ushahidi.

“Askari walikuta hali ya eneo hilo ni shwari na upelelezi ulianza mara moja ambapo majalada mawili ya uchunguzi yalifunguliwa moja la madai ya Chadema na lingine la madai ya DC,”  kudhalilishwa alisema.

Alitoa wito kwa vyama, viongozi wao, wanachama na wafuasi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi hususani katika kipindi hiki cha mchakato wa uchaguzi mdogo jimbo la Igunga.

Chadema walia na maadili
Katika hatua nyingine Chadema imewasilisha malalamiko dhidi ya Mkuu huyo wa Wilaya kwa Mwenyekiti wa Kamati ya maadili ya uchaguzi kufuatia kuitisha mkutano katika eneo la mkutano la chama hicho wakati wa kampeni za uchaguzi.

Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila, alisema kuwa mkuu huyo wa Wilaya amevunja sheria ya maadili ya vyama vya siasa na Serikali wakati wa kampeni ambayo inamtaka ofisa wa Serikali kutokutumika na au kujihusisha na kampeni za vyama vya siasa.

Alisema kuwa katika nyaraka walizomkuta nazo mkuu huyo wa Wilaya ni kufanya zoezi la kuweka wasimamizi wa vituo na waelekezaji katika uchaguzi kitendo ambacho ni hujuma ya uchaguzi na kinyume cha sheria.

“Kwa sababu ya makosa haya, tunataka kamati yako imwite Mkuu wa Wilaya na aeleze kwa nini amefanya makosa hayo na aadhibiwe kwa mujibu wa sheria ya maadili ya uchaguzi,” alisema.

Alisema wamepeleka nakala ya malalamiko hayo kwa Kamanda wa polisi wa wilaya, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kamanda wa polisi Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Jeshi la polisi nchini na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Kigaila alisema nyaraka zote walizomkuta nazo mkuu huyo wa Wilaya watazipeleka katika balozi za mataifa yote nchini na katika mifumo yote ya Serikali ili waelewe nini kinatendeka.

Ofisi ya msimamizi
Wakati hayo yakitendeka, Ofisa Uchaguzi wa Jimbo la Igunga, Martha Bayo, alisema kuwa hakuwa alipata taarifa za kitu gani Mkuu huyo wa Wilaya alikuwa anafanya, lakini kimaadili kama alikuwa hafanyi shughuli za mhadhara basi alikuwa hana tatizo lolote.

“Hatuwezi kulitolea ufafanuzi, DC alikuwa anafanya shughuli zake za kiserikali na wale wengine walikuwa na mkutano ila hatujapata taarifa rasmi,” alisema Bayo.


Kuhusu ratiba alisema kuwa jana Chadema walikuwa na mkutano saa 4 hadi saa 6 katika Kata ya Mbutu na wakati huohuo, walitakiwa wawe na mkutano katika Kata ya Isakamaliwa.

Waandishi wakosa uvumilivu
Katika mkutano huo baadhi ya waandishi wa habari walionekana kukosa uvumilivu baada ya kuonyesha waziwazi itikadi zao na kuanza kujibizana wenyewe kwa wenyewe juu ya mambo ambayo majibu yake yalipaswa kutolewa na Kamanda wa Polisi.

Waandishi hao walionekana kuuliza maswali mengine ambayo yalikuwa hayahusiani na polisi kitendo ambacho kilifanya waanze kujibizana wenyewe mbele ya Mungulu.

Kiravu ailamu Chadema
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Rajabu Kiravu, amesema kitendo cha Chadema kumkamata Mkuu wa Wilaya ya Igunga na kumweka chini ya ulinzi wao ni uhuni.Kiravu alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza kwenye mkutano ulioandaliwa na tume hiyo na viongozi wa vyama vya siasa nchini.

Alisema kitendo cha Chadema kumkamata Mkuu huyo wa Wilaya ni uhuni, kwani hata kama alikuwa amefanya kosa, walipaswa kufuata taratibu za kisheria."Walitakiwa wafuate taratibu, hawawezi wakajichukulia hatua za kumkamata. Kama alikuwa amevunja sheria walitakiwa wampeleke kwenye tume ya maadili," alisema Kiravu na kuongeza:

“Ule ni uhuni tu, kama kosa limetendeka kuna taratibu zake, Ifike mahala watu tuheshimiane huu, utaratibu wa kukamata umetoka wapi?” alihoji.

Kwa mujibu wa Kiravu, uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga haufanyi shughuli za kiserikali kusimama na Mkuu huyo wa Wilaya alikuwa akitekeleza majukumu yake ya kiseriakali, hakuna kosa.

“Uchaguzi haimanishi shughuli za Serikali zinasimama. Serikali ipo na inaendelea na majukumu yake kama kawaida," alisema Kiravu.Kiravu alisema majina ya mawakala yanapaswa kuwasilishwa kwa wasimamizi wa uchaguzi siku saba kabla ya siku ya kupiga kura hivyo kanuni za uchaguzi huo mawakala wa vyama vya siasa wanatakiwa kula kiapo cha kutunza siri siku tatu kabla ya siku ya uchaguzi.

“Kutokuwepo kwa mawakala hakutazuia mchakato wowote kuendelea,” alisisitiza Kiravu

Mwenyekiti wa Mkutano huo, Jaji Mstaafu Mary Longway, alipiga marufuku mawakala wa vyama vya siasa kuorodhesha majina na namba za kadi za wapigakura wakati wa la kupiga kura.

“Vilevile ni marufuku kwa mgombea, chama cha siasa au wakala kupiga kampeni siku ya uchaguzi kwani mwisho wa kupiga kampeni ni s
iku moja kabla ya siku uchaguzi,” alisema Longway. Chanzo: Gazeti Mwananchi

Thursday, September 15, 2011

Makamu Wa Pili Wa Rais Balozi Seif Idd Apokea Ubani Kutoka PPF ili Kufariji Watu Waliopatwa na Maafa ya Kuzama na Meli ya M.V Spice Islanders.

Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Pencheni ya mashirika na taasisi za umma Bw, William Erio akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hundi ya Sh, Milioni kumi kusaidia mfuko wa maafa wa Zanzibar kufuatia ajari ya meli ya Mv. Spice Islanders iliotokea hivi karibuni
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifafanua jambo mara baada ya kupokea hundi ya sh, milioni kumi kutoka kwa uongozi wa mfuko wa pencheni ya mashirika na taasisi za umma PPF kusaidia mfuko wa maafa wa Zanzibar kufuatia ajali ya mv spice. Pichani kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw William Erio akiwa na ofisa uhusiano wake Bibi Lulu Mengele
----
Na Othman Khamis Ame Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amepokea ubani kutoka kwa Uongozi wa Mfuko wa Pencheni ya Mashirika na Taasisi za Umma Tanzania {PPF } ili kufariji watu waliopatwa na maafa ya kuzama na Meli ya M.V Spice Islanders.
 
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio alimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Hundi ya Jumla ya shilingi milioni kumi Kusaidia mfuko wa Maafa Zanzibar unaoratibu shughuli zote za Maafa Zanzibar. 


Bwana William amesema Maafa yaliyowapata wananchi hao yamegusa Taasisi yao na Jamii yote ya Watanzania. Amewataka waliokumbwa na Mtihani huo kuwa na subira katika kipindi hichi kigumu cha Janga hilo. Akipokea msaada huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Balozi Seif Ali Iddi amezipongeza Taasisi na Jumuiya zote ndani na nje ya Nchi zinazoendelea kutoa misaada yao. Balozi Seif amesema misaada inayoendelea kutolewa inaashiria mshikamano uliopo kati ya Serikali, Taasisi tofauti pamoja na Wananchi.

JK Ampokea Rais Wa Visiwa Vya Comoro


1. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais wa Umoja wa visiwa vya Comoro Dr.Ikililou Dhoinine katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo mchana.

2. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Umoja wa visiwa vya Comoro Dkt.Ikililou Dhoinine muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana(Picha : Freddy Maro).

ni ccm hawa !

Katibu wa Taifa wa Uchumi na Fedha wa CCM, Mwigulu Nchemba, akihutubia wananchi wa kijiji cha Siimbo jimboni Igunga katika mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo




Picha na Victor Makinda wa Mjengwablog

Wednesday, September 14, 2011

Pat Rice asema Arsenal inajengeka

Meneja msaidizi wa Arsenal Pat Rice, anaamini sare dhidi ya Borussia Dortmund katika mechi ya kwanza ya patashika za Ligi ya Ubingwa wa Ulaya ni muelekeo mzuri wa timu hiyo kuanza kubadilika msimu huu.
Robin van Persie
Robin van Persie
Arsenal walionekana wameshinda mechi hiyo na kuzoa pointi tatu katika Kundi F hadi dakika ya 88 ambapo Ivan Perisic aliisawazishia Dortmund.
Lakini Rice, alipoulizwa iwapo Arsenal sasa imeanza kubadilika alisema: "Sana tu.
"Inaonekana ni hivyo, hasa ushindi dhidi ya Swansea siku ya Jumamosi, ndio tulianza msimu. Wachezaji tulionao ni wazuri, wazuri sana, ni wachezaji wazuri sana." Aliongeza Rice.
Arsenal walikuwa na hali ngumu hasa robo ya msimu huu kufuatia kuyumbayumba katika mechi za ligi baada ya kutoka sare na Newcastle na baadae wakapoteza mechi dhidi ya Liverpool na Manchester United - ambapo katika uwanja wa Old Trafford walibugizwa mabao 8-2.
Hata kufuzu kwa Arsenal katika Ubingwa wa Ulaya walipoishinda Udinese kwa jumla ya mabao 3-1, bado timu ilikuwa ikiyumba.
Hata hivyo mwishoni mwa dirisha la usajili, wakati Cesc Fabregas na Samir Nasri walipouzwa na wakawasajili Per Mertesacker, Mikel Arteta na Yossi Benayoun, mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu ya England walipoishinda Swansea, Rice anaamini Arsenal sasa ipo katika mchakato wa kujengeka.
Na kocha huyo amekuwa na kauli ya matumaini kufuatia sare dhidi ya Dortmund.
Robin van Persie alionekana kuifagilia njia ya ushindi Arsenal katika mechi ya ufunguzi ya kundi la F kwa kumalizia vizuri pasi aliyotanguliziwa na Theo Walcott lakini bao maridadi la Perisic likawanyima Arsenal pointi tatu.
Naye kocha wa Dortmund Jurgen Klopp amesema timu yake ilistahili kupata sare baada ya jitahada kubwa walizofanya.
"Ilikuwa ni mechi nzuri, lakini wakati mwengine kandanda ndivyo ilivyo," alisema Klopp. "Tulicheza vizuri, vizuri sana kwa muda wote wa dakika 90.Chanzo ni www. bbckiswahili.com

BAADA YA KUTUPIWA VIRAGO WANACHAMA VIGEUGEU , TEGETE AWA BUBU



WAKATI mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, akiwa bubu kuizungumzia adhabu yake ya kusimamishwa kwa mwezi mmoja, baadhi ya wanachama wa klabu hiyo wamepinga nyota huyo kupewa adhabu hiyo.

Uongozi wa Yanga, juzi ulitangaza kumsimamisha kwa mwezi mmoja mchezaji huyo kwa madai ya utovu wa nidhaumu aliyouonyesha wakati wa mazoezi ya timu hiyo hivi karibuni mbele ya kocha wake Mganda, Sam Timbe, kwenye uwanja wao wa Kaunda.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kwa njia ya simu leo Tegete alisema kuwa hivi sasa hawezi kuzungumzia tukio, hadi hapo atakapokuwa sawa.

“Sitaweza kuzungumza chochote juu ya hilo, labda siku nyingine endapo nitakuwa sawa, ila kwa sasa siwezi sema chochote,” aliongea mchezaji huyo na kukata simu.

Kwa upande wao, baadhi ya wanachama wa Yanga, walitoa maoni yao juu ya suala hilo la kumfungia nyota huyo wakati kwa sasa inaburuza mkia katika msimamo wa Ligi Kuu bara, wakidai ilitakiwa kamati ya ufundi kukaa na kujadili kwa kina suala hilo na sio kuchukua uamuzi wa haraka kama huo ambao ni tatizo kwa timu.

“Suala la kumchukulia Tegete maamuzi ya haraka ni kumvunjia heshima na ni maamuzi yasiyo ya busara, kwani Yanga ina taratibu zake, hivyo kamati ya nidhamu ilitakiwa kukaa na wahusika wote wawili, ambao ni Tegete na Sam Timbe ili kuzungumzia suala hilo la utovu wa nidhamu ambalo linamkabili nyota huyo dhidi ya kocha, kabla hawajatoa adhabu hiyo,” alisema mwanachama Saidi Bakari.

Naye mwanachama Charles Shinyambala alisema kwa sasa klabu inakabiliwa na mambo mengi, kuanzia kwenye suala la migogoro kwa viongozi na kuburuza mkia katika ligi, hivyo badala ya kamati kukaa kwanza na kulifanyia kazi suala hilo la Tegete, imetoa uamuzi wa moja kwa moja ambao hauna faida kwa timu na klabu kwa ujumla.

Aliongeza kuwa kitendo hicho ni tatizo kubwa kwani kuna mechi ambazo atazikosa na mchango wake ni muhimu katika timu, hivyo kamati ilitakiwa kukaa kwanza kabla ya kutoa uamuzi.

Monday, September 12, 2011

Benki ya Maendeleo ya Afrika Yaipa Serekali Ya Tanzania Msaada Wa Kiasi Cha Bilioni 133

Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(kushoto) akibadilishana hati ya msaada wa kiasi cha bilioni 133 na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) Tonia Kandiero(kulia) (leo) mjini Dar es salaam kwa ajili ya miradi ya kilimo na elimu nchini.
Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(katikati) akijibu maswali ya waandishi wa habari (leo)mjini Dar es salaam mara baada ya kupokea hati ya msaada wa kiasi cha bilioni 133 kutoka kwa Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) Tonia Kandiero(kulia) kwa ajili ya miradi ya kilimo na elimu nchini.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam