Monday, April 30, 2012

IKULU:Rais Jakaya Kikwete Awasili Tanga


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa ka furaha na Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyaakzi Tanzania (TUCTA) Bw Nicholaus Mgaya  leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mamia ya wakaazi wa jiji la Tanga leo April 30, 2012 baada ya kuwasili kuwa mgeni rasmi kesho katika sherehe za Mei Mosi,Picha na IKULU

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akabidhi Mchango Alioahidi Kwa Zanzibar One Taarab

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Mchango wa Shilingi Milioni Moja, Mkurugenzi wa Kikundi cha Zanzibar One Taarab Ustadhi Abdulla Ali{ Du } kufuatia ahadi yake aliyoitowa 21/4/2012 wakati wa kilele cha Maadhimisho ya kutimia miaka mitano ya Kikundi hicho yaliofanyika katika Ukumbi wa Bwawani , makabidhiano hayo yamefanyika Ofisi ya Makamu Vuga,.Picha na Hassan Issa-Ofisi ya Makamu wa Pili Wa Rais Zanzibar

TAHADHARI YA MVUA KUBWA...





AZAM WALIVAA TOTO LA YANGA LENYE NGUVU ZA SIMBA LEO


John Bocco Adebayor wa Azam kushoto, je leo ataingarisha Azam?
KAMA kuna mechi ambayo Azam ina umuhimu mkubwa basi ya leo dhidi ya Toto Africans ina umuhimu wake katika mbio za kuelekea kwenye ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. 

Azam ina pointi 53 inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi nyuma ya vinara Simba wenye pointi 59, hivyo kama Azam itashinda leo itafikisha pointi 56 na itakuwa na mechi moja mkononi dhidi ya Kagera Sugar Jumamosi, hivyo ikishinda itafikisha pointi 59 na kuomba Simba ifungwe na Yanga Jumamosi ili zihesabiane uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa kuamua bingwa wa msimu huu. 

Lakini kama Toto Africans ikiifunga ama kutoka sare na Azam leo itakuwa imeitangazia ubingwa Simba kabla ya ligi hiyo kumalizika, hivyo mchezo wake wa Jumamosi dhidi ya Yanga utakuwa wa kukamilisha ratiba. 

Kutokana na mazingira hayo mchezo wa leo utakaofanyika Uwanja wa Azam Chamazi utakuwa wa ushindani mkubwa kutokana na timu zote mbili kuuchukulia umuhimu mkubwa kwa vile Toto Africans yenye pointi 26 inashika nafasi ya tano kutoka mkiani ikiwa pia haipo salama sana kwenye zile timu zilizopo kwenye hatari ya kushuka daraja. 

Tayari Simba wametangaza azma yao ya kuiunga mkono Toto leo na jana Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga aliwatangazia mashabiki wa Simba Uwanja wa Taifa waende Chamazi wakashuhudie Toto anavyomfunga Azam.

Habari zisizo za kuaminika zinasema Toto wamepewa sapoti kubwa ya maandalizi na Simba kwa ajili ya mchezo wa leo.Chanzo:http://bongostaz.blogspot.com/

TUNATOA POLE KWA CHADEMA NA WANACHAMA WAKE WOTE KWA MSIBA ULIOWAPATA...


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Usa-River, wilayani Arumeru mkoani Arusha, Msafiri Mbwambo (32) ameuawa kinyama kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.Mamia ya wakazi wa Jiji la Arusha na Wilaya ya Arumeru jana, walifurika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru, kushuhudia mwili wa Mbwambo ambaye pia, alikuwa fundi ujenzi .Mbwambo aliuawa na watu wasiojulikana baada ya kupigiwa simu kumwita majira ya saa mbili usiku, wakati akitazama taarifa ya habari eneo la Mji Mwema akiwa na watu wengine. Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi ameni.Chanzo:http://kizobrax.blogspot.com/

Rais Dk. Shein akutana na Mabalozi


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Saudi Arabia Nchini
Tanzania Hani Abdalla Mohammed  Mu'minah,aliyefika Ikulu Mjini
Zanzibar leo kujitambulisha kwa Rais.[Picha na Ramadhan
Othman,IKulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Saudi Arabia Nchini
Tanzania Hani Abdalla Mohammed  Mu'minah,aliyefika Ikulu Mjini
Zanzibar leo kujitambulisha kwa Rais.[Picha na Ramadhan
Othman,IKulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran Nchini Tanzania Mohsen Movahhed Ghomi.aliyefika Ikulu Mjini
Zanzibar leo kwa mazungumzo na  Rais.[Picha na Ramadhan
Othman,IKulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran Nchini Tanzania Mohsen Movahhed Ghomi.aliyefika Ikulu Mjini
Zanzibar leo kwa mazungumzo na  Rais.[Picha na Ramadhan
Othman,IKulu.]